Thursday, August 16, 2012

VITUNGUU MKOANI SINGIDA NA UCHUMI WA TANZANIA


Vitunguu ni miongoni mwa mazao ya biashara yanayolimwa mkoani Singida, wakulima na wafanya biashara kwa kipindi kirefu wamekuwa wakilima zao hili na kuliuza maeneo mbalimbali ndani na nje ya nchi, Hata hivyo bado zao hili linakabiliwa na changamoto mbalimbali ikiwa ni pamoja na kukosekana kwa soko la uhakika pamoja na wakulima kukosa pembejeo; Serikali na mashirika yanawajibu wa kusaidia kupatikana kwa soko na matumizi mbadala ya vitunguu ama kwa kusindikwa na kupata soko nje ya nchi. Picha na. Doris Meghji


Na, Doris Meghji
Singida
Jumla ya shilingi billion 85,216 zimepatikana kutokana na biashara ya zao la kitunguu mkoani Singida katika kipindi cha fedha cha mwaka 2011/2012 ambapo tani 42,608 zilivuna na kuuzwa licha ya changamoto za maji na pembejeo zinawakabili wakulima na wafanyabiashara wa zao la kitunguu

Kaimu katibu tawala msaidizi huduma za uzalishaji mkoa wa Singida Bwana Charles Kidua ametoa takwimu hizo ofisini kwake juu hali ya uzalishaji wa zao hilo la kitunguu kuwa limekuwa likiongezeka mwaka hadi mwaka ambapo kwa kipindi cha misimu mitatu cha mwaka 2008/2009 tani 15,156 zilizalishwa,mwaka 2009/2010 tani 15,525 mwaka 2010/2011 tani 17 ,344 na mwaka 2011/2012 ya tani 42,608 zilizalishwa.

Aidha amesema zao hilo la kitunguu likiwa ni moja ya mazao ya biashara mkoani hapo limeweza kuajiri zaidi ya kaya 19,200 kutoka katika wilaya mbili za Iramba na Singida katika vijiji vya Msange, maghojoa,kinyeto,puma na kinyangighi kwa wilaya Singida huku wilaya ya Iramba ni vijiji vya Kaselya, Mwanga, Ilunda, Iguguno, Misigiri na Dominiki

Zao la vitunguu ambalo ni miongoni mwa mazao ya biashara katika mkoa wa Singida ambao pia hulima alzeti na kuzalisha mafuta ya alizeti, vitunguu pekee huajiri zaidi ya kaya 19,200 mkoani Singida

Hata hivyo wafanyabiashara wa zao hilo la vitunguu mkoani Singida wameilalamikia hali ya biashara ya zao hilo kuwa ya msimu kutokana na uzalishaji wake unaotegemea msimu wa mvua pekee hivyo wameiomba serikali kuwachimbia visima vya maji na mabwawa ya maji ili kuwa na upatikanaji wa maji ya uhakika na ilimo cha zao hilo kuwa endelevu na sio la kutegemea msimu wa mvua pekee.

“tulikuwa tunaomba msaada wa serikali kwa sababu wanasema sasa hivi ni kilimo kwanza wangetuangalia labda na sisi kutusaidi kuchimbia maji na sisi ili tujiendeleze kwa ajili ya kilimo cha kisasa kwa sababu kilimo cha msimu wa mvua ni kilimo cha bahati nasibu. ”alisema makamu Mwenyekiti wa soko hilo na mkulima wa zao la kitunguu Bwana Julius Majalo ambapo upatikanaji wa maji ya uhakiki utandeleza biashara ya zao hilo kwa kutunza soko la vitunguu kuliko ilivyo sasa kwa soko la zao hilo kuwa la mkoa wa singida pekee ukilinganisha na kipindi cha msimu ambapo Kenya, Uganda,Rwanda,Burundi Kongo na sudani huwa wateja wao.

Naye mwenyekiti wa madalali wa soko hilo Bwana Abrahaman Abdalah aliongelea suala la changamoto ya pembejeo za kilimo hasa za zao hilo la kitunguu kutokuwa na maduka ya ruzuku hasa mbolea kuuzwa kwa bei ya shilling 85,000/= “unaona mtu anajitahidi kulima heka mbili tatu atahitaji labda mifuko kumi ya mbolea (10) ambayo ni shilling laki nane na elfu hamsini (850,00/) tutalima kweli? tungeomba serikali ya mkoa ya singida itusaidie ituwekee hata na sisi wakulima ituboreshee pembejeo kwa kuwa na maduka ya ruzuku alisisitiza mwenyekiti huyo wa madalali sokoni hapo.

Katika kujibu changamoto hizo katibu tawala msaidizi wa huduma za uzalishaji mkoani singida Bwana Charles Kidua amesema katika kuendeleza kilimo serikali ya mkoa wa singida huwashawishi wakulima wa kitunguu kuungana katika vikundi ili wafike mahala wao wenyewe kuchimba visima."kuna baadhi ya maeneo tumewashawishi vijana wakulima kuungana kwenye vikundi na wamechimba visima ikiwa pamoja na kunua pambu ya kuvuta maji kwa ajili ya umwagiliaji na wengine wamenufahaika kutokana na skimu za umwagiliaji kwa zao la mpunga. Serikali haiwezi kumfikia mkulima mmoja mmoja."alisema bwana Kidua.

Aidha kwa suala la pembejeo za kilimo amesema katika kipindi cha mwaka huu wa fedha jumla ya tani 3 za mbolea yaminjingu kwa ajili ya kupandia na tani tano za mbloea ya urea kwa ajili ya kukuzia zimetengewa bajeti ikwa ni pamoja na nusu tani ya mbegu ya kitunguu ya aina ya Red Bombay katika mwaka huu wa fedha.

Kuhusu suala la kuboresha mazingira ya soko hilo Kidua amesema halmashauri ya manispaa ya singida imetenga bajeti ya kukarabati soko hilo katika kipindi hiki cha bajeti kwa kuwajengea paa ikiwa ni pamoja na sakafu ili waweze kuhifadhi vizuri vitunguu vyao.
Hata hivyo bwana Kidua amewataka wafanyabiashara hao kuzingatia suala la sheria ya vipimo kwa kutotumia ujazo maarufu kwa jina la lumbesa linalopunja mapato ya mkoa na mkulima kwa ujumla.

1 comment:

Anonymous said...

uko juu nastori imetulia.