Monday, August 27, 2012

MANYONI WAJITOKEZA KUANDIKISHWA-SENSA


 
Mkuu wa wilaya ya Manyoni mkoani Singida Bibi Fatuma Toufiq akitembelea moja ya kaya wakati za zoezi la sensa
Doris Meghji Jumatatu

Manyoni – Singida

Zoezi la sensa ya watu na makazi wilayani Manyoni linaendelea vizuri licha ya changamoto mbali mbali zilizojotokeza kwenye utekelezaji wa zoezi hilo katika baadhi ya vitongoji na vijiji juu ya suala la mipaka kati wilaya ya Uyui, Bahi,Sikonge na Manyoni

Mkuu wa wilaya ya Manyoni Bi Fatuma Toufiq ametoa taarifa hiyo wilayani humo jana mara baada ya kutembelea baadhi ya maeneo na kujua hali ya zoezi hilo limekwendaje

Bi Toufiq amesema kuhusu suala la mipaka katika vijiji vilivyoko mpakani kati ya wilaya yake na wilaya za Uyui,Bahi na Ikungu limetatuliwa kwa vijiji hivyo kuhesabiwa kuwa viko manyoni kutokana na ramani za kuhesabia maeneo (EA) zinavyoonyesha kwa makarani wa sensa ya watu na makazi wilayani humo

Aidha amesema katika wilaya yake wananchi wengi wameitikia zeozi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa sensa ya watu na makazi wa madodoso yote kwa kutoa taarifa sahihi kwa makarani huku akiwataka wananchi kutohujumu zoezhi hilo kwa kutoa ushrikiano kwa makarani wa sensa

Amesema “Ni kaya mmoja nilivyopewa taarifa kuna mtu alikataa kuhesabiwa akidai yeye ni muislam,lakini baada ya kuelimishwa na karani wetu alikubali kuhesabiwa kwa hiyo mwandishi hilo ni kaya moja ambayo alijitokeza mtu asiyetaka kuhesabiwa na kutatuliwa” alisema Mkuu huyo.

Hata hivyo mkuu huyo wa wilaya amesisitiza wananchi kuendelea kutoa ushrikiano kwa makarani hao wa sensa ili kufanikisha zoezi hilo la sensa ya watu na makazi litakalodumu kwa muda wa siku saba huku wilaya hiyo ikiwa na jumla ya kata thelathini.

Mwisho

No comments: