Sunday, August 19, 2012

EID MUBARACK WAUNGWANA



Mkurugenzi wa makampun ya Buhanzo Interprises na Standard voice Ltd Bw. James Japhet Daud pamoja na mkurugenzi wa Standard Radio fm Singida Bw. Prosper Laurent Kwigize wanawatakiwa waislam kote duniani maadhimisho mema ya siku ya EID EL FITRI

HII NI SIKU MUHIMU ya kujipongeza kwa siku 30 za mfungo mtukufu wa ramadhan, lakini pia ni siku ya kutafakari juu ya mwenendo mpya wa maisha baada ya kujinyima kutokula kwa mchana kutwa na kwa siku 30, hii si kazi ndogo wapo walioanza wakamaliza, wapo walioishia njiami kwa kufunga siku chache lakini pia wapo walioshindwa japo kuthubutu kufunga hata kwa siku moja

Mwenyezi Mungu awabariki wote na kuwapa moyo wa huruma, upendo, ujasiri na tafakari itakayowawezesha kuwa na mwenendo mwema wa maisha kwa kuepuka ubaguzi wa kidini, chuki na fitina zisizo na msingi wala tija

Mungu ibariki Tanzania, Mungu wabariki watu wote

Amen

No comments: