Tuesday, August 21, 2012

VILOBA VINATAFUNA NGUVU KAZI YA TAIFA


“Nimeteseka sana, nimetengwa sana, na nimeumizwa sana pamoja na kuwaumiza wenzangu, yote haya ni kwa sababu ya matumizi ya madawa ya kulevya, pombe kali hasa viloba hadi akili yangu ikaharibika nikajikuta nimekuwa mwehu nikitembea hovyo mitaani, kutukana na hata kupigana, hakika kwa sasa ninalo funzo kwa vijana wenzangu”

Hii ni Kauli ya kijana mmoja kutoka Dar es salaam ambaye sasa anatibiwa na kutunzwa katika kijiji cha Marumba wilayani Kasulu ambako alifikishwa na ndugu zake miezi kadhaa iliyopita baada ya kuugua ugonjwa wa akili na sasa akili yake japo kwa mwendo wa kinyonga inaanza kurejea.

Matumizi ya pombe kali VILOBA ni moja ya chanzo cha vijana wengi kuwa na matatizo ya akili na hata kupoteza afya ya mwili pia, si ajabu kuwakuta wapenzi na wanywaji wa viloba wakiwa maumbile yaliyokonda na kuchoka, kuungua midomo na hata kunyonyoa nywele, kukosa uwezo wa kufikiri na mwili kukosa nguvu

Si ajabu kumkuta kijana mpiga viloba akitetemeka mwili kila wakati anaposhika au kubeba chochote mikononi mwake, wengu wanashindwa hata kufanya kazi yoyote

Taifa limepoteza nguvu kazi kutokana na viloba na ulevi mwingine wa kupindukia pamoja na matumizi ya madawa ya kulevya,

Hii ndiyo sababu shirika la kitawa la BROTHERS OF CHARITY liliamua kuanzisha kitengo cha afya ya akili na kuanza kutoa tiba ya magonjwa hayo pamoja na matunzo ya kijamii na kisaikolojia kwa wagonjwa wa akili maarufu kama WEHU.

PICHA



No comments: