Sunday, August 12, 2012

SOKA LA VIJANA AFRIKA MASHARIKI NA KATI



Mwezi July mwaka huu Burundi ilikuwa mwenyeji wa mashindano ya mpira wa miguu kwa vijana chini ya miaka 20 kutoka katika taasisi za mafunzo ya soka (Accademy) za afrika mashariki ambayo huandaliwa na taasisi ya Rollingstone ya Arusha Tanzania

mkoa wa Makamba nchini Burundi ndio ulioandaa mashindano hayo kwa usimamizi wa mbunge wa Jimbo la Makamba Mhe. Kanal Mstaafu Revelian Ndikuriyo ambaye pia ni Senetor katika Serikali ya Peter Nkurunziza

Takribani timu 18 kutoka Afrika Mashariki zilikutanika mkoani Makamba nchini Burundi, Tanzania ilipeleka timu 7,, Burundi timu 6, DRC timu 3 na Uganda timu 1,

Aidha nchi za Rwanda na Kenya hazikuleta timu kutokana na sababu mbalimbali ikiwezo wanafunzi kuwa katika mitihani ya elimu ya msingi na sekondari.


Mlinda mlango wa timu ya Ecofoot Sud Kivu aliyezuia mikwaju ya penati na kuwawezesha timu yake kuibuka kidedea

katika mashindano hayo timu ya ECOFOOT SUD KIVU ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Congo -DRC ndiyo iliyoibuka kidedea baada ya kuchapa timu ya Coastal Union ya Tanga Tanzania bao 5-3 kwa njia ya mikwaju ya pelnat

Ushindi wa tatu ullikwenda kwa timu ya wafunga buti ya RUVU Shootinog ya Tanzania inayomilikiwa na Jeshi la Kujenga taifa



Waziri wa Vijana, Utamaduni na michezo wa Burundi akikabidhi kombe kwa mshindi wa kombe la ECAYFA, Timu ya ECOFOOT YA KIVU KUSINI ndio waliolitwaa, kushoto ni Kanal mstaaf Revelian Ndikuriyo mwandaaji wa mashindano mwaka 2012, mkoani Makamba nchini Burundi, kulia ni kocha wa timu ya ECOFOOT SUD KIVU
Aidha mashindano yote yalisimamiwa na taasisi ya kunoa marefaree (waamuzi) ya TWALIPO YOUTH SOCCER FOUNDATION ya Jeshi la Wananchi wa Tanzania JWTZ chini ya Kanali Chacha
Listone Hiraly mwamzi aliyechezesha mechi ya fainali kati ya Coastal Union na Ecofoot Sud Kivu, kijana huyu ni miongoni mwa waamuzi machachari wa soka wanaonolewa na academy ya JWTZ nchini Tanzania ya TWALIPO YOUTH SOCCER FOUNDATION



Mwandishi wa habari kutoka Standard Radio alikuwa mwalikwa na ililipoti kila kilichojili katika mtanange huo uliodumu kwa takribani wiki tatu.

kwa kuwa watu wengi wa afrika mashariki hawakuweza kusikiaoji au kuona yaliyojiri huko Burundi, mtandao huu unakuletea baadhi ya picha zilizopigwa siku ya fainali

MASHABIKI NA WAPENZI WA SOKA


No comments: