Friday, August 10, 2012

WAISLAMU NA SENSA

PICHA; Shekhe Masoud Kikoba, shekhe mkuu wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma nchini Tanzania
Kigoma
Shekhe wa wilaya ya Kasulu mkoani Kigoma, Shekhe Masoud Swed Kikoba, ametoa wito kwa waislamu wote kujitokeza katika zoezi la sensa ya watu na makazi itakayofanyika kuanzia August 26 mwaka huu na kukubali kuhesabiwa kwa manufaa ya maendeleo ya jamii na taifa la Tanzania
Wito huo umetolewa leo katika ibada ya ijumaa iliyofanyika katika msikiti mkuu wa ijumaa (masjid el jumaa) mjini Kasulu ukisomwa na katibu wa wilaya mzee Mtoa
Katika walaka huo, Shekhe Kikoba amebainisha kuwa sensa ni jambo muhimu kwa Tanzania na si mara ya kwanza kwa watanzania kuhesabiwa na hakuna dosari yoyote inayozuia waislamu kushiriki
Shekhe Kikoba amepinga vipeperushi vinavyosambazwa vikiwashawishi waislamuu kutoshiriki sensa na amewataka waislamuu kuvipuuza kwani yanayozungumzwa ndani yake hayana msingi wowote kwa waislamu Tanzania
Aidha ameunga mkono tamko Mufti wa Tanzania shekhe Issa bin Shaabani Simba alilotoa katika katika kikao cha july 16 mwaka huu kikihudhiriwa na mashekhe wa mikoa na wilaya zote Tanzania bara, lililowataka waislamu kujitokeza kuhesabiwa kama raia wengine wa Tanzania
Katika hali iliyowashangaza waislamu wilayani Kasulu, vipeperushi vyenye ujumbe wa kupinga sensa vilikutwa vimedondoshwa maeneo mbalimbali ya msikiti, hali iliyolazimu shekhe wa ilaya hiyo kutoa ufafanuzi na kuwataka waumini kupuuza ujumbe wa vipeperushi hivyo.
Aidha katika ibada hiyo aliwaasa waislamu kuzingatia imani na itikadi harisi ya uislamu na kuwatakia mfungo mwema wa mwezi mtukufu wa Ramadhani, na kuhimiza kuwa kufunga kuendane na kutimiza matakwa ya Mwenyezi Mungu na mtume Muhamadi SAW.


No comments: