Wednesday, August 8, 2012

VIONGOZI WA DINI MKOANI SINGIDA



Na, Doris Meghji
Singida

Viongozi wa dini mkoani Singida wameiahidi serikali kutoa ushrikiano katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kutoa elimu kwa waumini wao ikiwa ni pamoja na utoa tahadhari kwa watu wanaotaka kuvuruga zoezi la sensa kwa waumini wao 
Wakitoa maoni mbali mbali kwenye kikao chao na Mwenyekiti wa sensa mkoa wa singida Dr. Parseko Kone ambaye ni mkuu wa mkoa wa singida jana kilichofanyika katika ukumbi wa mikutano wa jengo la ofisi ya mkuu wa mkoa  wasema zoezi la sensa ni muhimu kwa maendeleo ya mkoa wa singida na nchi kwa ujumla hivyo watawaelimisha waumini wao ili waweze kushiriki vizuri zoezi hilo la sensa linalotarajiwa kufanyika Agosti ishrinini na sita mwaka huu.

Kwa upande wa viongozi wa dini ya kiislamu wamemuhakikishia mkuu wa mkoa kuwa watawaelimisha waumini wao kushiriki zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kutoa taarifa sahihi na za kweli na kuwataadhalisha juu ya wanaharakati wanaotaka kuvuruga zoezi hilo wasio utakia mkoa wa singida kwa kusambaza vipeperushi vinavyowakataza kushiriki sensa ya watu na makazi.

Katikakati ya kikao hicho suala la maombi likatawala ili kuweka kikao hicho katika uangalizi wa Mwenyezi ambapo mchungaji Jackoson Matola wa kanisa la AICT singida aliongoza maombi kwa kukemea watu wasio na mapenzi mema na nchi yetu na kuombea amani na utulivu uendelee kutawala miongoni wa Tanzania.

Hata hivyo mkuu wa mkoa wa singida Dr. Parseko  Kone aliitisha kikao hicho lengo ni kuomba viongozi wa dini kuhamasisha waumini wao kushiriki vyema katika zoezi la sensa ya watu na makazi kwa kuwa wao ni sehemu yenye nafasi kubwa kiimani kwa waumini wao na kutaadharisha mtu yeyote atakaye hujumu zoezi hilo atashitakika.
“mimi nadhani sijawatwisha nzigo mzito ambao ni kinyume na imani zetu,nimewaita kimkoa ili iwe katika mafundisho yenu katika ibada zenu kuhamasisha watu wakijitokeza kuhesabiwa ” Dr. kone aliwaomba viongozi hao.

Naye Victor Mkama mratibu wa msaidizi wa sensa ya watu na makazi mkoa wa singida amesema maandalizi ya zoezi hilo yanaendelea vizuri ambapo Agosti tisa makalani wa sensa wa dodoso refu watapatiwa mafunzo kwa kipindi cha siku kumi  (10) huku mafunzo ya dodoso fupi yatakuwa ya siku saba (7) yanayoanza kesho mkoani singida
Mwisho.

No comments: