Monday, September 3, 2012

SINGIDA NA KAGERA KUUNDA MTANDAO WA HABARI


Na Evarista Lucas

Singida

Uongozi wa Klabu ya Waandishi wa habri Singida(SINGPRESS); imeuomba uongozi wa Klabu ya waandishi wa habari Kagera kuwa mtandao wa mahusiano ambao  utasaidia katika kubadilishana mawazo haswa kwa upande wa kiutendaji.

Akizungumza kwenye hafla fupi ya kuagana iliyofanyika katika eneo la Bukoba Pub kati ya wajumbe kutoka Singida na baadhi wanachama wa KPC; mwenyekiti wa SINGPRESS Bwana Seif Takaza alisema , “Mimi naona tusiishie hapa tu bali tuunde mtandao wa mahusiano kati yetu na ninyi wanaKagera. Natumaini kuwa mtandao huu utaleta mabadiliko makubwa sana na kuwa mfano wa kuigwa na Klabu zingine.”

Ziara hii ni utekelezaji wa mpango mkakati uliowekwa na Muungano wa Klabu za Waandishi wa habari Tanzania (UTPC) katika mkataba uliotiwa saini na viongozi wa Klabu wanachama ambapo pia wanachama wamekuwa wakinufaika na mafunzo mbali mbali yanayoendelea kutolewa na UTPC.

Katika ziara hiyo  ya siku tatu iliyowajumuisha viongozi watatu na wanachama watatu wa SINGPRESS ; wajumbe hao walipata fursa ya kubadilishana uzoefu wa kiutendaji kupitia mahojiano ya hapa na pale  na kubwa zaidi wajumbe hawa walipenda kujua kuhusu vyanzo vya mapato vya KPC.

“Sisi tuna mradi wa steshenari(kutoa kopi) ambao unatuingizia kiasi cha shilingi laki moja na ishirini kwa mwezi. Pia tumeshawahi kuomba miradi mbali mbali huko nyuma na tukapata shilingi ukiwemo mraadi uliohusu kuripoti mambo ya sheria na jinsi ya kuripoti kesi za rushwa ambapo mradi huo uligharimu kiasi cha shilingui milioni ishirini na saba za Kitanzania kutoka tasisi ya kuzuia na kupambana na rushwa Tanzania(TAKUKURU) na pia mfuko wa kusaidia jamii(The Foundation for Civil Society).”  Alisema Mwenyekiti wa KPC Bwana John Rwekanika.

Rwekanika alifafanua kuwa kwa upande wao wameunda kamati ndogo ya miradi ambayo kazi yao kubwa ni kubuni miradi na kuiwasilisha katika kamati ya utendaji amabapo inabarikiwa. Pia Bwana Rwekanika alieleza kuwa wajumbe wa kamati hiyo wamekuwa wakipata asilimia kidogo kutoka kwenye miradi wanayoipata ikiwa nikuwatia moyo wa kuendelea na shughuli hiyo.

Naye katibu mtendaji wa SINGPRESS Bwana Abby Nkungu alitaka kufahamu  mikakati waliojiwekea  KPC kuepukana na na utegemezi wa UTPC. “Tuko  mbioni tunataka kujenga jingo la kibiashara ambalo litasaidia kutuingizia kipato ni adha kubwa kukaa unaomba omba.” Alisisitiza Rwekanika

Kwa upande wake katibu mtendaji wa KPC BwanaPhinias Bashaya alisema; “ Mwaka  juzi tuliendesha mradi  wa shilingi milioni arobaini na mbili  kuhusu suala la wananchi kutokujitokeza kupiga kura. Katika kradi huo pia tuliokoa kiasi cha fedha ambacho kilitusaidia kununua mashine ya kuburuza(fotokopi).

Kwa upande wao wanachama wa SINGPRESS(waliokuwa katika ziara hiyo) wameipongeza KPC kwa uataratibu mzuri waliojiwekea katika suala zima la utendaji na pia kuimarisha mahusiano kati yao na wadau wa habri mkoani hapo.

“Tunajitahidi kupunguza migogoro kati yetu na wadau  haswa linapokuja suala la mialiko.” Alisema Mwekahazina wa KPC BibiL ilian Lugakingira na kuongeza kusema kuwa migogoro kati ya wadau na waandishi wa habari iantokea sana kwenye  mialiko kwahiyo wanakuwa makini sana kuchagua waandishi makini ili kuepusha migogoro.

No comments: