Friday, September 28, 2012

JOTO LA UCHAGUZI LAPANDA - CCM IRAMBA

Na.   Phesthow   Sanga
Iramba, Singida

Chama Cha Mapinduzi {CCM} Wilaya  ya  Iramba  Mkoani  Singida,Kinajiandaa  Kufanya  Uchaguzi  wake  Mkuu  wa  ngazi  ya  Wilaya  septemba 30- Mwaka huu  kwa  Nafasi  ya Mwenyekiti  wa Wilaya, pamoja  na  Nafasi ya  {NEC}Taifa.
Katibu  wa  Wilaya  ya  Iramba  Mathias  Shidagisha  amewataja  wagombea  kwa  Nafasi  ya Mwenyekiti   wa  Wilaya Ambao  majina  yao Yamerudishwa  kutoka  Halmashauri  kuu  ya  ccm Taifa, ni  pamoja  na  Charles  Mkumbo Makala ,Moses  Nalogwa  Kitonka ,na  Mwenyekiti  ambaye   muda  wake Unaisha  Wilson Nico Msengi .
Shidagisha  amewataja  Wagombea  Wengine   Wa nafasi  ya  Halmashauri kuu  ya  ccm Taifa {NEC} Kuwa  ni   Joseph  Gerson  Mlewa ,Michael Shankolo Kitundu,  na  Aliyekuwa  Mbunge wa  jimbo la  Iramba Magharibi  Juma Hassan Killimbah.
Aidha   Katibu huyo  wa  ccm  Iramba  Ameeleza  kuwa   Nafasi  zingine  6  zinazo tarajiwa  kufanyiwa  Uchaguzi  ni  pamoja  na Katibu Siasa na Uenezi Wilaya  Nyenye  Wagombea  Watatu  kati ya  hao ni  Daudi Amos Madelu ,Wazaeli Nahuva Maja,na Moses Nalogwa  Kitonka.
Nafasi  nyingine  ni  ya  Katibu Uchumi  na  Fedha  Wilaya  nayo yenye  Wagombea  watatu  Ambao ni Charles  Mkumbo  Makala ,Jen  Henry  Mtata, pamoja  na  Zacharia Elias Mkoma  .
Aliwataja  Wajumbe  wengine  wanaogombea  Ujumbe  wa  Mkutano  Mkuu  wa  Taifa  ni  pamoja  na  Mkuu wa Wilaya  ya I ramba  Yahya  Nawanda ,Nafasi  Inayogombaniwa  na wagombea  wapatao  14.
Nafasi  nyingine  ni Wajumbe  wa Halmashauri kuu  ya Wilaya  Ambayo  Lina  kundi  la Wanawake  lenye  Wagombea  Wawili  kundi  Lingine  ni la Wazazi   Wagombea  Watano  na kundi  Jingine  ni la Vijana  Lenye Wagombea Watano pia .
Mathias  Aliwataja  Wajumbe Wengine  Watano   wanaogombea  Ujumbe  wa  Mkutano  Mkuu wa  Mkoa  ni  Marimu  Zabron  Rajabu,  Juma Swalehe Mhampa,  Humphrey Timotheo Shango, Chanima Hamud  Seifu,pamoja  na   Mathayo  Shango  Nguli.
Aidha  wajumbe  Wengine  wa Halmashauri  kuu ya Mkoa  toka  Iramba  ni Rehema Mssa  Mkasa ,Kinota Omary Khamis  {JB},Timothy  Wilson  Lyanga,Jane  Henry  Matata,  Elimamba Msafiri Lula, na  SaidRamadhani Tyunu .
Aidha Katibu wa Wilaya  Mathias,  Amewaeleza  Wagombea  Pamoja na  Wapiga  kura  kujihadhari  na  Tabia  ya  kutoa na kupokea  Rushwa  kwani wao  Wameandaa  VYombo  vyote  vya Usalama  kupambana  na  Changamoto  hiyo  kwa kila  Mtu  atakaye  jihusisha  na Mtandao huo.
Hivyo Mtu yeyote asije   kuulalamikia  Uongozi  kama  Atapatikana  na tatizo  hilo  la kutoa na kupokea  Rushwa ,na Amewaomba  Wajumbe  wote ambao  ni Wapiga  Kura  siku  hiyo  ya tarehe 30  kujitokeza  kwa  Wingi  ili Waweze  kumliza  kazi hiyo  iliyobakia  ya kupata  Viongozi  wa Ngazi ya Wilaya.
                                                       MWISHO.

No comments: