Friday, September 14, 2012

APANDISHWA KIZIMBANI KWA KUJERUHI MAMAYE

Na Doris Meghji
Singida

Kijana mmoja mkazi wa kijiji cha mangua manispaa ya Singida Shabani Abdalah (42) amepandishwa kizimbani kwa shitaka la kumjeruhi mama yake mzazi.


Katika shitaka hilo lililosomwa mbele ya hakimu wa mahakama ya mwanzo Ipembe Bwana Moses Msanya ilielezwa mahakamani na mlalamikaji bi Hadija Hamisi (65) ambaye ni mama mzazi wa mshitakiwa kuwa tukio hilo lilitokea mwezi wa ramadhani mwaka huu.


Kesi hiyo ya jinai N0 519/2012 ambaye iko katika hatua ya kusikilizwa.mlalamikaji aliieleza mahakama hiyo kuwa tukio hilo lilitoke majira ya saa moja usiku kuwa mshitakiwa alifika nyumbani kwao akionekana amelewa pombe alianza kutoa lugha ya matusi huku akimtishia mama yake kumtaka kwa panga


Kwa mujibu wa mlalamikaji mshitakiwa Sahabani Abdalah aliendelea kufanya fujo kwa mzazi wake akiwa na wajukuu wake wawili hatimaye akamkata mama yeke mkono na kumjeruhi mara tatu katika mkono wake wa kushoto


Hata hivyo mlalamikaji alidai mbele ya mahakama kuwa mshitakiwa anatabia ya ulevi na ugomvi wa mara kwa mara uliosababisha mama yake na wajukuu wake wawili wanaoishi pamoja kulala kwa majirani kutokana na vitisho vya silaha,jambo amabalo akiripoti kwa viongozi wa serikali ya kijiji bila mafanikio


Akimhoji mlalamikaji ,Mshitakiwa huyo alitaka kujua iwapo mlalamikaji alijua sababu za kumjeruhi kwake ,ambapo mlalamikaji hakujua chanzo cha kujeruhiwa

Katika ushaidi wake, mjukuu na shahidi wa pekee wa mlalamikaji mwenye umri wa miaka kumi na miwili(12) aliieleza mahakama kwamba mshitakiwa ambaye ni mjomba wake alikuwa na mazoea ya kufanya fujo mara kwa mara akiwa amelewa pombe na kuwafukuza usiku na kulala nje kwa majirani.

Hata hivyo kesi hiyo imehairishwa hadi septemba 27 mwaka huu kwa ajili ya kusikilizwa upande wa utetezi

No comments: