Monday, September 3, 2012

MAKALA YANGU, SIKUAMINI HATA KIDOGO


Na Evarista Lucas
Singida
Nakumbuka  vizuri  siku ambayo nilifurahi kupita kifani nilippopokea simu kutoka kwa rafiki yangu kipenzi Halima  “Jiandae best siku ya Jumatano utaenda kutia saini mkataba.” Kabla  hata hajamaliza nilimuuliza mkataba wa nini tena swahiba? Bila kusita akanambia “ Umepata  ajira, unaenda kutia saini mkataba baina yako na Klabu.”

Kiukweli nilifurahi sana ukizingatia kwamba nilikaa nyumbani kwa muda mrefu toka nilipohitimu mafunzo yangu ya shahada ya awali ya mawasiliano ya umma  katika Chuo kikuu cha Mtakatifu Agustino Mwanza. Si lengo langu haswaa kuwahabarisha haya yote lakini napenda mjue yafuatayo.

Mnamo  mwaka 2011 mwezi siukumbuki vizuri; badhi ya Klabu (viongozi) za waandishi wa habari Tanzania zilisaini hati ya makubaliano kati yao na Muungano wa Klabu za waandishi wa Habari Tanzania(UTPC).

Kwa upande wa Klabu ya waandishi wa habari Singida(SINGPRESS0; mkataba huo ulisainiwa na aliyekuwa katibu mtendaji wa SINGPRESS wakati huo Bi Doris Meghji  sambamba na Mwenyekiti Mch. Immanuel Barnaba

Hati hiyo ililenga kuzisaidia Klabu wanachama  kwa kuwapatia vifaa, mafunzo,kulipia kodi ya pango kwa mwaka, kufunga mtandao wa intaneti, vocha za intaneti kwa mwaka na kulipia sehemu  ya mshahara wa mratibu wa Klabu na pia mafunzo mbali mbali yenye lengo la kuwaongezea uwezo wa kitaaluma.

Ama kwa hakika wanachama wa SINGPRESS wamenufaika vilivyo na mpango mkakati huu wa UTPC. Kwakuwa  tangu mkataba huo kusainiwa tayari Klabu hiyo imeshalipiwa fedha kwaajili  ya kodi ya pango la ofisi na pia wanachama wanaendelea kunufaika na mafunzo yanayotolewa kwa awamu nne tofauti.

Mbali na hilo ;hivi karibuni viongozi watatu (Mwenyekiti, Katibu Mtendaji na Mwekahazina) na wanachama watatu wallipata fursa ya kufanya ziara ya kimafunzo katika Klabu ya waandishi wa habari Kagera(KPC). Lengo kubwa la ziara hii ilikuwa ni kubadishana  uzoefu wa kiutendaji.

Kwa upande mmoja naweza nikasema ama kwa hakika tumevuna na kupata zaidi ya kile tulichokuwa  tumekitaraji. Nasema hivyo kwa mantiki zifuatazo; kwanza tumepata kujifunza jinsi wenzetu wa Kagera walivyonufaika kupitia miradi waliyoomba ambapo tulidadisi namna walivyoomba na kufanikisha kupata mikopo hiyo na pia kufahamu wafaddili waliofadhili miradi hiyo.

Mara tu baada ya kurejea kutoka Kagera viongozi walijadili namna ambavyo wataweza kubuni miradi mbali mbali ya kuiongezea kipato Klabu kwa kuomba uhisani kutoka taasisi na mashirika mbali mbali.

“Mwenda bure si mkaa bure”  Hatimae nasi tulipata fursa ya kutembelea eneo la kihistoria ambapo vita vya Kagera mwaka 1978/1979 vilipigwa(Mutukula)mpakani mwa Tanzania na Uganda.  Kwakuwa ilikuwa ni mara yetu ya kwanza kufika mkoani Kagera; tulifurahi zaidi kwani tuliongeza elimu tuliyokuwa nayo aidha kwakusimuliwa kuhusu vita vya Kagera ama kwa kusoma sasa tulijionea pia mabaki ya kanisa lililopigwa mabomu na Nduli Idd Amin Dadaa.

Hatukuishia hapo tu; kwani ujio wetu mkoani Kagera ulikuwa wa kipekee sit u kwa viongozi wa Klabu ya waandishi wa habri Kagera; bali pia hata kwa baadhi ya waandishi na baadhi ya vituo vya matangazo(Redio) kama ilivyokuwa kwa redio Kasbante fm.

“Tunawakaribisha sana hata kwa  ziara binafsi au ya wote. Tumefarijika sana na ujio wenu na nnafikiri kuwa Klabu zetu zitaleta mabadiliko makubwa katika tasnia ya habari. Pia tunaomba kupata mwakilishi kutoka huko.” Alisisitiza mtendaji mkuu wa redio kasbante Bwana Richard Leo.

Nae Afisa Masoko wa redio Kasbante Bi Abella Kamala aliwaasa wanahabari kushirikiana haswa katika suala zima la uhuru wa vyombo vya habari na pia kudumisha upendo na mshikamano miongoni mwa waandishi wa habari.

               

No comments: