Thursday, September 13, 2012

UMASIKINI NOMA - WIZI WAMPELEKA JELA

NA  PHESTHOW  SANGA; 
SINGIDA  



Mmoja  katika  kijiji  cha Manga  katika  Manispaa ya  singida ,Selemani  Mussa( 20) Amepandishwa  kizimbani  katika Mahakama  ya  Mwanzo  Utemini  Kujibu Tuhuma  ya Shambulio na wizi .

Katika  kesi ya  jinai  na 538 ya Mwaka  huu 2012 Inayoendelea  kusikilizwa  katika Mahakama  hiyo iliyofunguliwa  spt 6 Mwaka  huu  inaeleza ;

Mnamo Augasti  27 mwaka huu  Majira  ya saa  10;jioni katika kijiji cha Manga ,Selemani  na Wenzake wawili  ambao hawakufanimika,Walimvamia, Juma (40) kumpiga  nakuchuwa  Simu moja  na Pamoja na fedha taslim u Elfu 40.000.

Akitoa Ushahidi wake  Mbele ya Hakimu wa mahakama  ya Mwanzo U-temini  Ferdinand M.Njau ,kuwa yeye  ni  Mkaazi  wa wa kijiji cha Uhamaka kijiji  jirani  cha Manga  kumfuata  Mke wakewe  ndipo alipovamiwa  na Selemani na wenzake wawili  ambao hakuwatambua .

Aliongeza katika Ushahidi  wake kuwa  kitendo cha kushambuliwa  yeye  na watu hao  ni kumkomesha  kwani katika  hao watatu  mmoja wao  Alikuwa na mahusiano ya ki-Mapenzi  na mkewe hivyo  walikuwa  wanamkomesha  ili aache kumfuata;  kwani  mke wake hataki kukaa nyumbani  na Anakaa Nyumbani  kwao  kwa mda mrefu sasa .

Aidha  alisema  kuwa  Baada  ya kushambuliwa  ndan i kwa  Mkwewe  alienda  kwa  Ofisa wa  kijiji na  kuomba Barua ya kwenda kituo  cha  Polisi  Singida kwa  ajili ya Barua na 3. Ya kwenda kutibiwa katika  Hospitalini  na Baadaye kuleta  shitaka  lake  Mahakamani  hapa  spt.6 Mwaka  huu.

Hata  hivyo  kesi  hiyo Imepangwa  Kuendelea  kusikilizwa  tena katika  Ushahidi  upande wa  Mlalamikaji spt 19 mwaka huu.

No comments: