Wednesday, September 12, 2012

CHAMA CHA MAPINDUZI CHAKAMILISHA CHAGUZI ZA JUMUIYA


Mwenyekiti wa ccm Mkoa Jorum Alute akiwa na Mwenyekiti wa UWT wilaya Bi Yagi Kiaratu na pembeni yake ni msimamizi mkuu wa uchaguzi huo Bi Queen Mulozi mkuu wa wilaya ya Singida.


Na. Doris Meghji
Singida
Zikiwa chaguzi mbali mbali za jumuhiya za chama cha mapinduzi ngazi za wilaya mkoani singida zimekamilika kufanyika wanachama wa jumuhiyia hizo wametakiwa kuchagua viongozi makini na wenye uwezo wa kuongoza ili kuhakikisha chama cha mapinduzi kinaendelea kushika dola

Mwenyekiti wa chama cha Mapinduzi mkoa wa Singida Bwana Jorum Alute ametoa rai hiyo mapema wiki hiki wakati akifungua mikutano mikuu ya chaguzi za jumuhiya hizo kwa kuaasa wanachama kuchagua viongozi watakao kuwa tayari kufa kwa ajili ya kukipigania chama cha mapinduzi ili kiendelee kushika dola hivyo viongozi watakao chagua kwenye chaguzi hizo wawe viongozi bora na makini watakao kikisaidia chama hicho kuendelea kushika dola kupitia mafiga yake matatu ambayo ni UVCCM, UWT na

WAZAZI.

 

“viongozi mtakao wachagua watuhakikishie ushindi wa chaguzi za serikali za mitaa mwaka 2014 na uchaguzi mkuu wa mwaka 2015,hapa mjini tumeingiliwa na vyama vya upinzani kila mtu anafahamuzi,mtakao tuokoa ni ninyi, ni uchaguzi huu wa leo,mtachagua viongozi ambao wako tayari kufa na kupona kuhakikisha chama cha mapinduzi ili tuendelee kushika dola.Singida mjini mmchoka na amani tulionayo? Alisitiza kwa swali mwenyekiti Alute

Aidha alisitiza juu ya suala la umoja wa kitaifa ulioachwa na Baba wa Taifa mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Mwenyekiti huyo wa CCm mkoa wa Singida anasema “ Baba wa taifa alituachia umoja na mshikamano, umoja wa kitaifa bila kujali wewe ni rangi gani kabila gani na dini gani aliunda taifa la umoja wa kitaifa nchini Tanzania unaweza kuishi mahala popote na hakuna atakaye kuuliza wewe ni kabila gani na wenyeji wakukaribisha bila shida yoyote.

 

Sasa taifa limeanza kumeguka meguka watu wameanza kuingiza udini wameanza kuingiza umajimbo wanataka wakitawala wao warudishe majibo ambayo yalikuwa ya ukoloni lakini wanataka wao sasa ni kwamba warudishe majimbo kwa maana ni kwamba unarudisha ukabila kama mkuu wa mkoa awe mnyaturu au mnyiramba,kama ni mkuu wa wilaya awe mnyaturu au mnyiramba na wanataka hayo majimbo au kila mkoa mkoa uwe na wabunge wake lake na mipango ya maendeleo yatokane na rasilimali za mkoa wetu wa singida kwa sababau wao tayari wameshaendelea wanarasilimali zaidi kuliko sisi wana madini,wana mlima Kilimanjaro,wana kahawa wana mazao ya kudumu ambayo wanawaletea maendeleo

Hao sio watu wa kuaachia taifa hili” alisisitiza Mwenyekiti Alute

 

Hivyo aliwataka washikamane wachague viongozi bora na sio viongozi

Hata hivyo katika changuzi hizo kwa upande wa uchaguzi wa UWT wilaya ya singida mjini aliyeshinda nafasi ya uenyekiti ni Bi Consolata Mziray alipata kura 184 kati ya kura 294 zilizopigwa huku akiwashinda wagomba wenzake ambao ni Hadija Simba aliyepata kura 97 na Immaculata Ilanda Njiku mwenye kura 3 kati ya kura 274 zilizopigwa

 

Kwa upande wa wagombea nafasi mkutano mkuu wa UWT taifa ambao ni Jane Kishari mwenye kura 203,Bi Marium Kambi aliyepata kura 187,Bi Scola Marwa kura 167,Bi Aisharose Matembe kura 110, Bi Saidati Mziray Kura 42,Bi Hadija Simba kura 28, Bi Hamida Saidi kura 21 Bi Mwanahasha Hamisi kura 16 huku Bi Pili Athumani alipata kura 12 kati ya kura 294 zilizopigwa katika mkutano huo na kuwafanya Bi Jane Kishari mwenye kura 203,Bi Marium Kambi mwenye kura 187 na Bi Scola Marwa mwenye kura 167 kuwa wajumbe wa mkutano Mkuu wa UWT taifa kutoka jumuhiya hiyo wilaya ya Singida Mjini.

No comments: