Thursday, September 13, 2012

ELIMU YA KUPAMBANA NA UKIMWI YATOLEWA KWA WANAHABARI


Na. Halima Jamal

Bagamoyo-pwani

 

Kwa mara nyingine kituo bora cha redio mkoani singida (starndradiofm) kimejiongezea wigo wa uelewa kutokana na kupata mafunzo yanayohusu maswala ya UKIMWI na jamii yaliyofanyika Bagamoyo mwanzoni mwa mwezi huu.

Mafunzo hayo yaliyoandaliwa na shirika la TACAIDS kupitia shirika la GIZ yalishirikisha waandishi wa redio(prisenters) takribani 20 wakiwa wametoka sehemu mbalimbali za mikoa ya Tanzania.

Aidha lengo la kuwakutanisha waandishi hao ni pamoja na kuwapa uelewa  wa kutangaza vema dhana inayohusu uhusiano na maradhi ya UKIMWI  katika jamii inayotuzunguka kwa vyombo vya habari hasa redio.

Katika mafunzo hayo yaliyoendeshwa na mkufunzi mwenye uzoefu Dk Katanta Simwanza yalilenga hasa katika mfumo dume unaoendelea katika baadhi ya familia tunazotoka kuwa mwanaume ndio kichwa cha nyumba katika mahitaji ya kawaida

Katanta alisema kuwa familia nyingi maamuzi ya mwisho yanatolewa na baba,ambapo si sawa kuwa hata mama katika familia anaweza kutoa maamuzi ambayo yanaonekana kuwa sahihi.

''mfumo dume umegawanyika katika makundi matano,ambayo ni majukumu,maamuzi,madaraka,ushiriki pamoja na umiliki wa rasilimali''alisema Katanta.

Alifafanua kuwa katika majukumu ya mume na mke katika familia yanatokana na wanaume wengi kukataza wake zao kufanya kazi na kuwaambia wakae majumbani na kuwaletea wanachopata huko na kuwa mwanamke yule atakuwa anamuogopa mume wake hata akimsikia ana wanawake hawezi kumuuliza kuogopa hatapewa matumizi ya kila siku.

Alisema kuwa mwanamke anakuwa na jukumu la kulea watoto tu na kwa upande wa madaraka idadi kubwa ya familia hupenda kumuona mwanamke kuwa hafai kushika wadhifa wowote.

katika sehemu ya ushiriki Katanta lisema kuwa asilimia kubwa wanaume hawakubali kushiriki katika kuwasindikiza wake zao cliniki pindi wanapopata ujauzito.

Alisem katika suala ya umiliki wa rasilimali wanaume hupinga kabisa wanawake kumiliki bali wao tu ndio wanaopaswa kumiliki ardhi hizo.

Katanta alisema kuwa katika hayo yote ndio hupelekea maambukizi ya virusi vya UKIMWI kuendelea kusambaaa.

Hivyo basi waandishi wa habari hasa watangazaji wanatakiwa waeleze jamii kuwa mfumo huo kuwa na mbaya na athari zake ni kuwa malezi na makuzi kwa watoto wanaozaliwa mfumo huo unawapotosha bali kizazi hichi kinachokuja kiwe na uelewa mzuri kuhusu hilo.

Mafunzo hayo ya Siku tatu yalioanza oct5 na kumalizika oct7 mwaka huu yaliwakilishwa na Halima Jamal kutoka standardradio Singida.

No comments: