Friday, September 14, 2012

KKKT YAHIMIZA USHARIKA


Na, Daudi Nkuki

Singida

 

Ili ushirika upate hadhi ya kujitegemea, hauna budi kuonyesha uwezo wa kukidhi vigezo vyote vinavyotakiwa na kanisa la kiinjili la kilutheri Tanzania (kkkt)dayosisi ya kati.

 

Msaidizi Mteule wa Askofu wa KKKT Dayosisi ya Kati Mchungaji Spriani Yohana Hilinti’amebainisha hayo alipokuwa akizindua usharika mpya wa mazoezi wa msamaria mwema katika eneo la Getwanus wilayani Hanang

 

Vigezo hivyo ni pamoja na kuwa na uongozi kamili,akiwemo Mchungaji wa usharika ,jengo la kuabudia ,nyumba ya uchangaji na uwezo wa kimapato yasiyopungua shilingi 200,000/=kwa mwezi kwa ajili ya kuhudumia usharika ,jimbo la Dayosisi na KKKT yenyewe.

 

Kwa mujibu wa historia iliyotolwa kwa msaidizi mteule wa askofu,ibada ya kwanza ilifanyika April 21,1985 katika kijiji cha Getanuwas iliyohudhuriwa na wakisto wahamiaji 14 kutoka sehemu mbali mbali nchini.

Mtaa ulifunguliwa rasmi Julai 28,1985 na mchungaji Japhet Lalu kutoka ushirika wa Neema Mpipiti,ulioko wilaya ya Singida Vijijini ,ambalo ni eneo la Dayosisi ya kati.

 

Kwa bahati mbaya kijiji kilikumbwa na ghasia za vita vya kikabila ,baina ya wanyaturu na wabarabaig ,zilizowasambaratisha wahamiaji kukimbilia vijiji jirani

 

Baada ya vita kuisha walirudi tena kuendelea na shughuli za kanisa,ikiwa ni pamoja na wazo la kuanzisha ujenzi wa jengo la kuabudia mwaka 2000 hadi lilipokamilika mwaka 2010

 

Jengo hilo limgharimu shs.40,000,000/= lililojengwa kwa nguvu za wakristo na michango yao wenyewe bila kupata msaada wowote ,lina uwezo wa kuchukua watu 300 wakati mmoja.

 

Usharika wa msamaria mwema umetokana na mitaa ya Getanuwas na samaria yenye jumla ya wakristo 680. kati watu wazima 270 na watoto 410.pia ushirika umepata mchungaji mpya Japhet Nakomolwa Kidindima

 

No comments: