Thursday, January 31, 2013
MAJENGO HAYA YANAPASWA KUTUNZWA KAMA KUMBUKUMBU
JENGO LA ZAMANI LENYE HISTORIA KUBWA YA UKOLONI LINALOTUMIWA NA HALMASHAURI YA WILAYA YA IRAMBA MKOANI SINGIDA, NI MIONGONI MWA MAJENGO MUHIMU KWA HISTORIA YA TANGANYIKA
HOSPITALI YA RUFAA SINGIDA KUKAMILIKA
Majengo ya Hospitali ya Rufaa nayojengwa mjini Singida, hospitali hii inatarajiwa kusaidia kupunguza tatizo la wagonjwa kusafirishwa kwenda KCMC na Bugando pindi wanapohitaji matibabu ya utaalamu wa juu zaidi
Tuesday, January 29, 2013
DODOMA KUZIMA MITAMBO YA ANALOGIA
Mamlaka ya mawasiliano
Tanzania TCRA imekamilisha maandalizi ya kuzima mtambo wa mawasiliano wa
analogia na kuwasha mtambo mpya wa digital mkoani Dodoma.
Hayo yamesemwa na
Mkurugenzi wa utangazaji TCRA Bw. Habi Gunze wakati akizungumza na waandishi wa
habari jana ambapo amesema kuwa hatua hiyo imefikiwa baada ya maandalizi ya
kuwasha mtambo huo unaotarajiwa kuwashwa usiku wa alhamisi ya wiki hii
kukamilika.
Amesema mwezi mmoja
sasa umepita tangu jiji la Dar es salaam limehama kutoka mfumo wa analogia na
kwenda digitali hivyo kwa sasa ni zamu ya mkoa wa Dodoma na Tanga.
Naye Meneja wa TCRA Bw.
Innocent Mungi amewataka wakazi wa mkoani humo kuhakikisha kuwa wamenunua
ving’amuzi ili kuepusha usumbufu unaoweza kujitokeza.
Baadhi ya wakazi wa
mkoa wa Dodoma wameipongeza mamlaka husika kwa kufikia hatua hiyo wakati
wengine wakilalamikia gharama za matangazo kwani watatakiwa kulipia. EndS
MABINTI WASHAURIWA KUSUSIA NDOA DHIDI YA VIJANA WASIO NA NYUMBA BORA
Mkuu wa wilaya ya Mkalama Bw. Edward Ole Lenga (kulia) akisisitiza jambo kuhusu ujenzi wa nyumba wilayni humo na kuwataka wavulana wasikimbilie kuoa wakati wakiishi ndani ya Tembe, Tembe ni aina ya mjengo wa asili kwa wakazi wa mikoa ya kati, hususani Singida, Dodoma na sehemu ya miko aya Tabora na Shinyanga.
Serikali wilayani
Mkalama mkoani Singida imewataka wasichana kukataa kuolewa na wanaume ambao
hawajajenga nyumba za kisasa kama sehemu ya kuhimiza ujenzi wa nyumba bora
Ushauri
huo umetolewa na mkuu wa wilaya ya Mkalama Edward ole Lenga wakati akisoma
taarifa ya utekelezaji wa Ilani ya uchaguzi kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi
2012
Bw.
Lenga amesema bado wakazi wa wilaya hiyo mpya hawajawa na mwamko wa kujenga
nyumba bora na badala yake wanaendelea kuishi katika nyumba za asili maarufu
kama tembe
Amesema
nyumba hizo za asili si imara na zimekuwa zikihatarisha maisha ya wananchi hasa
nyakati za masika
Mkuu huyo wa wilaya
amebainisha kuwa serikali licha ya kuhimiza wananchi kujenga nyumba bora bado
mwitikio ni mdogo na hivyo kuwaelimisha wasichana na akina mama juu ya umuhimu
huo, ndiyo njia pekee ya kuleta mabadililo
WILAYA YA IRAMBA KUANZISHA CHUO KIKUU
Mkuu wa wiilaya ya Iramba Bw. Yahaya Nawanda (katikati) akitsoma taarifa ya utekelezaji wa ilani ya Uchaguzi ya CCM kwa kipindi cha mwaka 2005 hadi 2012. Kushoto ni Mbunge wa Iramba Mwigulu Nchemba na kulia ni Mkurugenzi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba Bi. Christine Midello.
Serikali kwa
kushirikiana na kanisa la kiinjili la kirutheli Tanzania dayosisi ya Kati
wameanzisha mchakato wa kujenga chuo kikuu katika mji wa Kiomboi wilayani
Iramba
Mkuu wa wilaya ya
Iramba Bw. Yahaya nawanda amebainisha hayo jana katika taarifa yake ya
utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2005/2012
Ameeleza kuwa kwa mwaka
wa masomo wa 2013/2014 chuo hicho kitaanza kudahili wanachuo wa shahada ya
kwanza ya ualimu kwa ajili ya chuo kikuu Kiomboi Iramba.
Bw. Nawanda amesema
kuanzishwa kwa chuo kikuu mkoani Singida kutasaidia kukuza kiwango cha taaluma
kwa shule za msingi na sekondari pamoja na kuongeza uwezekano wa ajira kwa
vijana.
MWIGULU NCHEMBA KUWASILISHA HOJA BINAFSI BUNGENI
Mbunge wa jimbo la
Iramba Magharibi na naibu katibu mkuu wa Chama cha Mapinduzi Bw. Mwigulu
Nchemba anatarajia kuwasiilisha hoja binafsi katika kikao cha Bunge
kinachoendelea mjini Dodoma
Akizungumza na Standard
Radio Bw. Nchemba ameitaja hoja hiyo kuwa ni kuitaka serikali kuanzisha mfuko
maalumu wa elimu ya juu
Amebainisha kuwa
Tanzania haina mfuko maalumu wa kuwasaidia vijana wanaojiunga na vyuo vikuu na
kwamba fedha zinazotolewa na bodi ya mikopo kwa sasa haina chanzo maalumu na
cha uhakika
Kuhusu tabia ya wabunge
kugeuza Bunge kama sehemu ya kurushiana maneno na kusababisha vurugu, Bw.
Nchemba amesema chama cha mapinduzi kimewaelimisha wabunge wake kupeleka hoja
za msingi kwa ustaarabu na kuepuka vurugu
Amesisitiza kuwa
Bunge ni mahali pa kwenda kujenga hoja za maendeleo ya wananchi na kwamba
chanzo cha vurugu zilizokuwa zikijitokeza mwaka jana Bungeni ni wabunge kuwa na
hisia za ubinafsi badala ya kufikiria taifa.
Sunday, January 27, 2013
BODA BODA WAPATA MAFUNZO YA UDEREVA
Mkuu wa chuo cha VETA Singida Afridon Mkhomoi, Akifafanua jambo wakati wa hafla hiyo ya kutunuku vyeti wahitimu wa mafunzo ya udereva wilayani Mkalama.
Picha na Nathanael Limu
Serikali wilayani
Mkalama mkoani Singida, imekipongeza chuo cha mafunzo ya ufundi stadi (VETA)
Singida, kwa uamuzi wake wa kuanza kuwafuata wateja mahali walipo, badala ya
kuwasubiri waje chuoni.
Pongezi hizo zimetolewa na mkuu wilaya hiyo, Bw Edward Ole
Lenga wakati akizungumza kwenye halfa ya kufunga mafunzo ya waendesha pikipiki
(Bodaboda) iliyofanyika Nduguti, makao makuu ya wilaya mpya ya Mkalama.
Katika hotuba ya Bw. Lenga iliyosomwa kwa niaba yake na mkuu
wa kituo cha polisi Mkalama Bw. Michael
Marwa, amesema uamuzi huo wa busara wa kumfuata mteja mahali alipo, una faida
nyingi ikiwemo ya kutoathiri shughuli za mteja
Katika hatua nyingine, mkuu huyo wa wilaya, ametoa rai kwa
wakazi wote wa wilaya ya Mkalama wanaomiliki na kuendesha pikipiki, magari au
vyombo vya moto, kujitokeza kwa wingi kujiandikisha katika kila kata, ili
waweze kuletewa mafunzo.
Awali
mkuu wa chuo cha VETA Singida Afridon Mkhomoi, amesema mafunzo yanayotolewa na
VETA yanalenga kukidhi sera ya nchi ya kuwawezesha vijana kujiajiri na kuwa
wajasiriamali.
245 PEOPLE HAVE DIED IN A FIRE
Photo By. BBC
At least 245 people have died in a
fire that swept through a nightclub in a university city in southern Brazil,
police and officials say.
Local media say the fire began when a band let off fireworks at the Kiss club in Santa Maria, Rio Grande do Sul.
Reports say panic spread as people tried to get out. Many victims reportedly died from inhaling toxic fumes or from being crushed.
The fire is now out and bodies are being removed from the scene.
President Dilma Rousseff, who cut short a visit to Chile and was returning to Brazil, said everything possible would be done to help the injured and the families of the victims.
I would also like to say to the Brazilian people and to the people of Santa Maria that we stand together at this time, and that even though there's a lot of sadness, we will pull through," she said, speaking from Chile.
In a tweet, the governor of Rio Grande do Sul, Tarso Genro, said it was a "sad Sunday" and that all possible action was being taken in response to the fire. He would be in the city later on Sunday, he added.
NAFASI ZA UWAKALA WA STANDARD RADIO
Tunapenda kukutangazia kuwa, STANDARD RADIO Inatoa fursa kwa wanaohitaji kuwa mawakala wetu katika maeneo mbalimbali kanda ya Kati, mkoa wa SIngida na maeneo ya jirani
kama unapenda kuwa wakala wetu tafadhari leta maombi yako.
By. Utawala
Saturday, January 26, 2013
BIASHARA YA MKAA MKOANI SINGIDA NA MSTAKABALI WA MAZINGIRA
WANANCHI mkoani Singida, wameshauriwa kuacha
biashara ya uchomaji mkaa, na badala yake waelekeze nguvu zao katika ufugaji
wa nyuki, kwa madai kwamba una faida zaidi kuliko biashara ya mkaa.
|
Wito huo umetolewa juzi na Meneja wakala wa huduma za
misitu Tanzania (T.F.S) wilaya ya Singida, Hashimu Kavito, wakati akizungumza
na waandishi wa habari juu ya mikakati inayochukuliwa na wakala huo,
kufanikisha malengo ya upandaji miti, mkoani hapa.
Alisema ufugaji wa nyuki gharama yake ni ndogo mno
ukilinganisha na ile ya uchomaji mkaa.
“Pia ufugaji wa nyuki licha ya kuwa hauna gharama
kubwa, unayo faida nyingi. Ufugaji wa nyuki unasaidia misitu isikatwe ovyo, bei
ya asali na nta, kwa sasa ipo juu mno",alifafanua Hashimu.
Meneja huyo, alisema kutokana na ukweli huo, mfugaji
wa nyuki anayo nafasi kubwa ya kuboresha uchumi wake, wilaya, mkoa na hata
taifa tofauti na muuza mkaa.
Katika hatua nyingine, aliwataka wananchi wabadilike
na kuanza kutambua kuwa miti ni sawa na mazao mengine yaliyozoeleka.
MOHAMED DEWJI AMWAGA MSAADA WA VITENGE SINGIDA
Na. Nathanael Limu
Alisema pamoja na vikundi hivyo, pia wajumbe wa
halmashauri mkuu ya matawi, wafanyabiashara wa kuku za kienyeji soko kuu,
boda boda na taasisi mbali mbali, zitanufaika na msaada huo.
|
“Lengo la kumwomba mbunge Dewji msaada huo wa vitenge,
ni kutaka kufanikisha sherehe hizo za chama kikongwe cha CCM kutimiza miaka
36.Chama kuendelea kuwa na mshikamano kwa kipindi chote cha miaka 36, ni jambo
la kujivunia na kupigiwa mfano”,alisema Duda.
Msaidizi huyo wa mbunge,alisema kwa hali hiyo, sherehe
hii muhimu, ni lazima nayo ipewe heshima ya aina yake ikiwemo wanaccm na
wapenzi wake, waonekane tofauti siku hiyo ya sherehe.
Katika hatua nyingine, katibu tawi la Ughaugha (CCM),
Hamisi Ramadhani, alisema msaada huo wa vitenge, ni mwendelezo wa misaada mingi
ya kimaendeleo anayotoa mbunge Dewji, jimboni kwake.
RAIA WA ETHIOPIA WAHUKUMIWA NCHINI TANZANIA
Na Nathaniel Limu
JUMLA ya raia 12 raia wa nchini Ethiopia,wamehukumiwa na mahakama ya wilaya
ya Singida,kulipa faini ya shilingi laki moja (100,000) kila mmoja baada ya kukiri
makosa mawili ya kuingia na kuishi ndani ya ardhi ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania bila kibali halali.
Pia mahakama hiyo,imeamuru basi la kampuni ya Mtei ya mjini Arusha T.797
CDZ lililokuwa limebeba Waethiopia hayo,likamatwe na kutaifishwa kuwa mali ya
serikali.
Raia hao wa Ethiopia ambao ni bado vijana wadogo na wengine ni wanafunzi wa
shule na vyuo, ni pamoja na Ahmed Mohammed Mahamud,Tazana Dijamo Walao, Mohammed
Abdi Osman, Abraham Nirato Shango, Adinan Abrahim Abdalah na Alamu Ayele Gabresekesie.
Weingine ni Muhidini Sufiani Ahmed, Tasfai Sutatu Kidisu, Yassin Mohammed Hassan,
Afandi Aden Suleiman, Ayele Liranso Gafuche na Pakala Agore Mancha.
Baada ya nwendesha mashitaka mwanasheria wa serikali Ahmed Seif kuwasomea
makosa hayo mawili ya kuingia na kuishini nchini bila ya kuwa na
kibali,washitakiwa wote kila mmoja kwa nafasi yake, walikiri kutenda makosa
hayo.
Kabla ya kutolewa kwa adhabu hiyo,mwanasheria wa serikali,Seif,aliiomba
mahakama hiyo kuwa iwape adhabu kali washitakiwa ikiwa ni njia moja wapo ya
kukomesha vitendo vya wahamiaji haramu kuingia na kuishi nchini bila ya kuwa na
kibali cho chote halali.
"Mheshimiwa hakimu vile vile naiomba mahakama yako itaifishe basi la
Mtei lililotumika kuwasafirisha wahamiaji hawa haramu ili kuwaogofya wenye
magari kuacha kusafirisha raia wa kigeni wasiokuwa na kibali halali cha kuingia
na kuishi nchini"alisema Seif.
Akitoa hukumu hiyo, hakimu mfawidhi kiongozi wa mahakama ya wilaya ya
Singida, Flora Ndale,alisema mahakama yake imezingatia yale yote yaliyoombwa na
upande wa mashitaka na utetesi na kufikia uamuzi wa kutoa adhabu ya kulipa
faini ya shilingi laki moja kwa kila mshitakiwa.
"Mahakama hii inawatia hatiani na kuwapa adhabu ya kulipa faini hiyo
ya shilingi laki moja kila moja na atakayeshindwa kulipa faini,atakwenda
kutumikia jela kwa kipindi cha miezi mitatu"alisema hakimu Ndale.
Hata hivyo,washitakiwa wote 12,kila mmoja wao alilipa faini hiyo ya
shilingi laki moja na hivyo kuachiwa huru.
Kwa mujibu wa mwanasheria wa serikali Seif, washitakiwa hao wamekamatwa January
17 mwaka huu alasiri katika eneo la kijiji cha Kititimo nje kidogo ya mji wa
Singida wakiwa wametokea mkoani Arusha wakielekea nchini Afrika kusini.
Friday, January 25, 2013
PARACHUTI KUTUMIKA MLIMA KILIMANJARO
Wakazi waishio jirani na mlima Kilimanjaro watanufaika na utalii wa
kuruka milima kwa maparachuti utakaofanyika kwa mara ya kwanza nchini, mwezi
februari mwaka huu.
Akizungumza na waandishi wa habari, afisa habari wa mamlaka ya Hifadhi
za Taifa Tanapa Bw. Pascal Shelitete amesema fedha zitakazopatikana kupitia
utalii huo zitabaki nchini na wananchi waishio jirani na mlima Kilimanjaro
watanufaika kupitia mradi wa utunzaji mazingira.
Mradi huo ni pamoja na shughuli zinazohusu masuala ya virusi vya
ukimwi, mradi wa maji safi na salama chini ya asasi za one foundation, water
International, na plant purpose.
Tukio hilo linatarajiwa kukusanya zaidi ya watalii mia moja kutoka
nchi ishirini na tano duniani, na imelenga kukusanya takribani shilingi bilioni
mbili za Kitanzania.
POLISI WAJENGEWA NYUMBA IRAMBA
Mkuu wa jeshi la Polisi mkoani SIngida ACP Linus Sinzumwa (katikati) akikagua ujenzi wa nyumba ya kuishi askari katika kituo cha polisi Misigiri wilayani Iramba , Ujenzi huo unatekelezwa na wananchi wa kata ya Misigiri ambao wameamua kufanya hivyo baada ya kukerwa na uharifu na kisingizio cha polisi kutokuwa na makazi.
MANSPAA YA SINGIDA YALAUMIWA KUTWAA ARDHI YA WANANCHI
Wakazi
wa vitongoji vya Mwamtanda na Mwaja kata ya Mandewa wameilalamikia halmashauri
ya Manispaa ya Singida kwa kutotimiza ahadi ya kuwalipa fidia waliyoitoa
wakati maeneo yao ya
ardhi yalipochukuliwa na serikali
kwa ajili ya upimaji wa viwanja vipya.
Wakazi
hao wamesema hayo jana wakati wakizungumza
na Mkuu wa wilaya ya Singida Bi. Queen
Mlozi, baada ya kutembelea vitongoji hivyo.
Wakazi
hao wamesema, wakati serikali inahitaji
viwanja waliahidiwa kuwa kila mtu atapewa kiwanja na kulipwa fidia jambo ambalo
halikutekelezwa, hali iliyopelekea
baadhi ya wananchi kukosa makazi.
Wamesema
baadhi yao wamekwenda katika ofisi za ardhi ili kutaka kupata maelekezo zaidi na kuonyeshwa
sehemu mbadala na kufuatilia fidia zao, badala yake wamepewa
barua za kutakiwa kuondoka katika maeneo yao.
Mkuu wa
wilaya ya Singida Bi.
Mlozi amewataka wakazi hao kuwa
na subira kwa kuwa suala hilo linatafutiwa ufumbuzi.
WANAJESHI WA RWANDA WATEKWA KAGERA
Wanajeshi wa
jeshi la Rwanda waliokuwa wakisafiri kutoka Kigari kwenda Dar es Salaam
wamenusurika kifo baada ya watu wanaotajwa kuwa majambazi kuliteka gari
walimokuwa wakisafiria
Tukio hilo
limetokea alfajiri leo majira ya saa 12:45 asubuhi katika kijiji cha KIkoma
Kata ya Lusahunga wilayani biharamulo moani Kagera
Katika tukio
hilo jumla ya magari matano yametekwa na watu wenye silaha nzito za kivita
Akizungumuza
Standard Radio kwa njia ya simu Diwani wa kata ya Lusahunga Bw. Amoni Mizengo
amesema, wanajeshi hao wa Rwanda walikuwa wakisafiri kwenda Dar es salaam
kununua magari.
Aidha askari
mmoja wa jeshi la polisi Tanzania Kituo Cha Nyakahura wilayani Biharamlo ni miongoni
mwa waliotekwa na kuporwa vitu mbalimbali
Mkuu wa
jeshi la polisi mkoa wa Kagera ACP Phillip Kallang amethibitisha kutokea kwa
tukio hilo na kwamba jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi ENDS
KATIBA IWATAMBUE WALEMAVU WA NGOZI
Wajumbe wa
kamati ya chama cha albino mkoa wa singida TAS, wamefanya semina ya mafunzo ya
siku mbili katika ukumbi wa kituo cha walimu nyerere katika manispaa ya Singida
yakuwawezesha kutambua haki zao na kutoa maoni kuhusu katiba wanayoitaka.
Akitoa
mafunzo hayo Bw. Godwel Mwamakula ambae ni mwanasheria ofisi ya kazi kwa mkuu wa
upelelezi wa makosa ya jinai mkoa wa singida amesema kuwa walemavu wa ngozi ni
lazima watambue haki zao za msingi, ili waweze kutoa maoni yao katika katiba
itakayoundwa.
Bw.
Mwamakula ameongeza kuwa katiba iliyopo haijaweka wazi haki anazohitaji kupata
mlemavu wa ngozi hivyo katiba ijayo lazima iundwe tume itakayochunguza na kuhakikisha viongozi wote wanatambua mahitaji
ya makundi maalum wanakuwa waadilifu na mahakama ipewe uhuru wa kusikiliza
madai ya haki za walemavu hao.
Akihitimisha
semina hiyo, Bw Mwamakula amesema kuwa ulinzi shirikishi na polisi jamii ni kwa
ajili ya usalama wa raia na mali zao, hivyo watumie fursa hiyo kutoa taarifa wakiwa
na tatizo lolote ili kuondokana na vitendo vya unyanyasaji katika maeneo
wanayoishi na kufikisha waliyopata
kwenye semina kwa wenzao.
Kwa upande
wao walemavu wa ngozi wamesema wanakabiliwa na changamoto mbalimbali kama vile,
ukosefu wa mafuta ya kulainisha ngozi zao, gharama za elimu, matibabu na kufanya
kazi ngumu. Wameiomba serikali kupitia katiba itakayoundwa kuangalia changamoto
hizo.
WAPANGAJI WA NYUMBA MKOANI SINGIDA WALALAMA
Baadhi ya
wapangaji katika manispaa ya singida
wamelalamikia wenye nyumba kwa kuwanyanyasa na kuwadharau kwani na wao
wanahitaji kuheshimiwa.ili waweze kuishi kwa huru kama watu wengine.
Hayo yamesemwa
na mmoja wa wapangaji Bi.Rehema mussa alipozungumza na standard radio ambapo
amesema kuwa wenye nyumba wamekuwa wakiwadharau wapangaji kwa kuwatolea kauli
chafu, kitendo kinachowafanya waishi
bila amani na kuwa na hofu wakati wote.
Naye Bw. Haruna
Issa amesema kuwa wenye nyumba ni lazima watambue kuwa wapangaji wanahitaji
kuthaminiwa kwani wengi wao walikotoka wana nyumba pengine nzuri kuliko hata
hizo.
Hata hivyo
ameongeza kwa kusema kuwa wenye nyumba lazima wawe na msimamo katika mapatano ili kuepusha usumbufu unaojitokeza
kutokana na baadhi yao kubadilisha kodi kinyume na maelewano baina yao na
wapangaji.
TANGAZO MAALUM KUTOKA STANDARD VOICE LTD
Tunapenda kukutangazia kuwa
kituo chetu cha Radio kiitwacho STANDARD RADIO FM sasa kimeanza kurusha
matangazo yake mkoani Singida
Miongoni mwa matangazo
yanayorushwa na Radio hii ni Taarifa za habari, Vipindi mbalimbali pamoja na
burundani ya Muziki mchanganyiko wenye ladha inayoendana na mahitaji ya
msikilizaji
Aidha vipindi vyetu pia
vinaandaliwa na watayarishaji mahili kwa kuzingatia uhitaji wa jamii, kisiasa,
kiuchumi, kijamii na kiutamaduni
Miongoni mwa vipindi
tulivyonavyo ni
· HOJA YA LEO
· UCHUMI WETU
· UKULIMA NA MAZINGIRA NA UFUGAJI
· UKIMWI
· ELIMU YETU
· HAKI NA USAWA
· ULIMWENGU WA MICHEZO
· UJASIRIAMALI
· WATOTO
· VIJANA NA UJANA
· UZEE NI TUNU
· WAJIBU WAKO
· AFYA NA UZAZI
Standard radio inasikika
katika masafa ya FM - 90.10 MHz na inasikika mkoa mzima wa Singida pamoja na
maeneo yafuatayo
1.
Igunga
2.
Nzega
3.
Uyui
4.
Kondoa
5.
Katesh
6.
Mbulu
7.
Manyara
8.
Bahi
9.
Hanang
na maeneo mengine jirani na
mkoa wa Singida
Tunakukaribisha kuitegea
sikio Radio Yako STANDARD RADIO FM Sauti ya Wasiosikika na tunakukaribisha
ulete habari, matangazo, maoni na maswali pia
Aidha tunao wawakilishi wetu kutoka mikoa ifuatayo KIGOMA, DODOMA, RUKWA, KAGERA, MANYARA na DAR ES SALAAM
SLP 62 SINGIDA
SIMU. 0786200518, 0787 592056, 0764243377
BARUA PEPE srfm2011@gmail.com
Tupo pia katika mitandao ya
jamii TWITTER na FACEBOOK
Waweza pia kututembelea katika
BLOG yetu kwa anuani ifuatayo www.standardradiofm.blogspot.com
STANDARD RADIO FM, SAUTI YA
WASIOSIKIKA
Wednesday, January 23, 2013
WATU WATATU WAFARIKI DUNI MKOANI KIGOMA
Na. Mwandishi wetu
Jeshi la polisi Mkoani Kigoma limebainisha kuwepo kwa Watu watatu wambao amefariki dunia katika matukio mawili tofauti
wilayani kasulu mkoani Kigoma kati ya Januari 21 na 22 mwaka huu likiwemo tukio
la mtu kujinyonga.
Kamanda wa polisi mkoani Kigoma ACP Frasser Kashai amebainisha hayo leo na kutaja kuwa
katika tukio la kwanza mtoto wa umri wa miaka 15, Sharifu Rajabu mkazi wa
kijiji cha Nyarugusu wilayani Kasulu alikutwa amejinyonga nyumbani chumbani
kwake nyumbani kwao kwa kutumia kamba ya chandarua.
Aidha katika tukio lingine kamanda Kashai amesema wakazi
wawili wa kijiji cha Kwaga wilayani Kasulu Bw. Paulo Hakani mwenye umri wa miaka
45 na bi.Prisca William mwenye umri wa miaka 23 wamefariki dunia baada ya
kupigwa na radi wakiwa shambani kwao Januari 22 mwaka huu kufuatia mvua kubwa
iliyokuwa ikinyesha.
EndS
POLISI KUYAFUNGA MAKAMPUNI YA ULINZI TABORA
Na. Moses mabula
KAMANDA
wa Polisi mkoani Tabora ACP Anthony Rutta amesema kuwa atayafungia kufanyakazi
makampuni yote ya ulinzi mkoani humo ambayo yanashindwa kutekeleza masharti
yaliyopewa na jeshi hilo.
Mkuu
huyo wa Polisi mkoa wa Tabora amesema kwamba jeshi la Polisi lilitoa masharti
kwa wamiliki wa makampuni yaho kuwa hayaruhusiwi kuajiri walinzi wasio
waadilifu ambao wamekuwa wakila njama za kufanya uharifu wa wizi kwenye taasisi
mbalimbali ambayo wameingia nazo mkataba wa ulinzi.
Akizungumza
na mwandishi wa habari ofisini kamanda Ruta alikiri kuwepo kwa baadhi ya
makampuni ya ulinzi ambayo hayafuati taratibu za ajira za walinzi huku akiapa
kuyashughulikia ipasavyo kwakuwa baadhi ya makampuni hayo yamekuwa yakiajiri
walinzi wasio na sifa na kukosa uaminifu.
Kuhusu
matukio ya hivi karibuni ya wizi uliofanyika katika Shirika lisilo la
kiserikali la Total Land care ambalo lilipata hasara ya zaidi ya shilingi
mil.kumi na tatu baada ya walinzi wa kampuni ya ulinzi ya Alliance Day &
Night la hapa mjini Tabora ambao wanadaiwa kula njama na kufanya wizi wa
kuvunja ofisi za Shirika hilo.
Kamanda
Rutta amesema bado Polisi wanaendelea na uchunguzi lakini mlinzi mmoja wa
kampuni hiyo anayefahamika kwa jina la Said Kayungilo alitoweka kabla ya kukamatwa.
Monday, January 21, 2013
KITUO CHA MABASI UBUNGO CHALETA BALAA
Watu watatu
wamejeruhiwa na magari ishirini na manne
kuharibika baada ya ukuta wa kituo kikuu cha mabasi yaendayo mikoani cha Ubungo
jijini Dar es salaam kuanguka leo
asubuhi katika eneo la kuegeshea magari.
Kamanda wa polisi mkoa
wa Kinondoni Bw. Charles Kenyela amesema ukuta hbuo umeanguka kufuatia kazi ya
ubomoaji inayoendelea katika eneo hilo. Amesema watu waliojeruhiwa wamepelekwa
hospitali kupata matibabu.
Kufuatia ajali hiyo
watu wametakiwa kuwa waangalifu katika eneo la kituo cha mabasi Ubungo, ili
kuepuka athari zinazoweza kutokea wakati zoezi la kuondoa magari yaliyoangukiwa
na ukuta, likifanyika
KANISA LA ANGLIKANA LAKIRI KUKABILIWA NA UKATA
Waumini wa kanisa la Anglikana mjini
Singida leo wamekumbushwa kuwa kutoa
sadaka ni sehemu ya ibada.
Akihubiri katika kanisa la Anglikana
la Mtakatifu Paulo, mwinjilisti Musa Njagamba amesema awali kanisa hilo
lilitegemea misaada kutoka kwa wafadhili hivyo waumini wanapaswa kujenga tabia
ya kutokuwa tegemezi bali wanapaswa kujitolea ili kuliendeleza kanisa lao.
Amesema neno la Mungu halihitaji
msaada kutoka nje bali waumini wanapaswa kubadili mienendo kwa kutoa sadaka ili
kanisa hilo liweze kujiendesha lenyewe.
CHADEMA WAWALALAMIKIA WANAWAKE
Mratibu wa sera za chama cha Demokrasia na Maendeleo CHADEMA
Mkoani Singida Bi Jesca Kishuwa amelalamikia baadhi ya wanawake mkoani Singida kutohudhuria katika mikutano ya hadhara hasa ya kisiasa.
Bi Jesca amesema hayo jana wakati wa mkutano wa hadhara
wa chama cha Democrasia na Maendeleo
(CHADEMA) uliofanyika katika viwanja vya stendi ya zamani ya mabasi mkoani
Singida.
Bi Jesca ameeleza kuwa licha ya idadi kubwa ya watanzania
kuwa na kundi kubwa la wanawake, bado akina mama wako nyuma kimaendeleo na
kiufahamu kutokana na kutojihusisha na masuaala ya kisiasa
MKUU WA MKOA WA SINGIDA ACHACHAMAA
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr, Parseko Kone ameonya tabia ya
baadhi ya maafisa wa serikali na vyombo vya habari kutoa taarifa zisizo sahihi
kwa wananchi
Dr. Kone amesema hayo jana katika hafla fupi ya kuuaga mwaka
2012 na kuukaribisha mwaka 2013, iliyofanyika katika chuo cha utumishi wa Umma
mjini Singida
Dr. Kone amesema hayo kufuatia vyombo vya habari kuripoti
habari ya uhaba wa chakula mkoani Singida, na kutaja kuwa takwimu zilizotolewa
katika habari iliyochapishwa na moja ya magazeti ya kil asiku si sahihi
Mwishoni mwa wiki, baraza la madiwani wilaya ya Singida
lilikiri kuwepo kwa uhaba mkubwa wa chakula na kuagiza uongozi wa halmashauri
hiyo kulitafutaia ufumbuzi mara moja
Friday, January 18, 2013
POLISI SINGIDA WAPATA PIKIPIKI KUIMARISHA ULINZI
ACP Linus Sinzumwa Kamanda wa polisi mkoa wa Singida
Mkuu wa jeshi la polisi nchini IGP Said Mwema ametoa
jumla ya piki piki 22 kwa jeshi la polisi mkoani Singida, kama sehemu ya
utekelezaji wa mkakati wa kuimarisha ulinzi nchini na kusogeza huduma za
usalama jirani na wananchi
Akitoa taarifa kwa vyombo vya habari mkuu wa jeshi
la polisi mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa amebainisha kuwa pikipiki hizo
zitasambazwa katika tarafa za mkoa huo
Kamanda Sinzumwa amebainisha kuwa piki piki hizo
zitakabidhiwa kwa askari wateule ambao watazitumia kwa ajili ya kufanya doria
na kuzuia uharifu katika tarafa ambazo watapangiwa pamoja na kuimarisha
ushirikiano baina ya raia na jeshi hilo
Mkuu wa mkoa wa Singida Dr. Parseko Kone,
anatarajiwa kukabidhi vyombo hivyo vya usafiri kwa jeshi hilo mapema wiki ijayo
MKUU WA MKOA SINGIDA ATOA AGIZO KWA WAKUU WA WILAYA
Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameagizwa
kuwajulisha wananchi juu ya utekelezaji wa ilani ya uchaguzi tangu mwaka 2005
hadi mwaka 2012, kupitia vyombo vya habari vinavyowafikia wananchi kwa urahisi.
Agizo hilo limetolewa hivi karibuni na Mkuu wa mkoa
wa Singida Dk. Parseko Ole Kone, wakati akitoa taarifa ya utekelezaji wa ilani
ya uchaguzi kwa waandishi wa habari ofisini kwake.
Dk. Kone amesema wakuu wa
wilaya wakifanya hivyo na wananchi kupewa fursa ya kutoa maoni yao, itakuwa ni
njia rahisi kufikisha taarifa kwa wananchi ambao nao watatoa maoni yao moja kwa
moja na kuhoji wataalam wa sekta mbali mbali juu ya utekelezaji wa ilani hiyo.
Wakuu wa wilaya zote mkoani Singida wameahidi kutoa
taarifa za utekelezaji wa ilani ya uchaguzi katika wilaya zao kutumia vyaombo
vya habari.
Subscribe to:
Posts (Atom)