Thursday, October 11, 2012

TOTO YALOWA KWA YANGA 3-1

Timu ya soka ya Dar Young African imeibugiza timu ya Toto African  ya Mwanza kwa jumla ya Mabao 3-1 na hivyo kuukata mzizi wa fitina uliokuwa umetanda jiji la mwanza ambako kila mnazi wa soka alikuwa akiitabiria Toto ushindi.

mabao mawili ya yanga yamepatikana kipindi cha kwanza cha mchezo na bao la kuididimiza Toto likitinga nyavuni kipindi cha pili.

Katika mtifuano huo ambao umechezwa katika uwanja wa CCM Kilumba jijini Mwanza, Toto walikosa penalt katika dakika 43 za mchezo na kupoteza matumaini ya ushindi ingawa kipindi cha pili walifanikiwa kujipatia bao hilo lililowapunguzia machozi waliyopata kipindi cha kwanza, hata hivyo Toto wameshindwa kufua dafu kwa Yanga ambayo  ilipachika bao la tatu na kuwavunja nguvu watoto hao wa Lock city

Mwandishi wetu Edson Raymond alikuwa shuhuda wa kichapo hicho cha watoto wadogo wa Dar es salaam na wenzao wa jiji la Miamba, Mwanza

No comments: