Sunday, October 21, 2012

WATUMA SALAAMU WATOA MISAADA KWA WATOTO VIZIWI


Na.  Boniface  Mpagape.

Chama cha watuma salaam kupitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini, kimetoa msaada  kwa watoto  viziwi wanaosoma katika shule ya msingi Tumaini iliyopo katika manispaa ya Singida.

Watuma salaam hao nchini  wametoa msaada wa vitu mbali mbali vikiwemo sabuni, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi na fedha taslim shilingi laki moja.

 Katika risala yao watuma salaam hao nchini wamesema  ni vyema pia kwa taasisi nyingine na watu wenye mapenzi  mema  nchini kuiga mfano wa kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji na kutoiachia jukumu hilo serikali pekee.  Wamesema misaada kama hiyo imetolewa pia katika mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Mbeya, Morogoro, Manyara, na Dodoma. Aidha wametoa wito kwa jamiii kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Bi. Christina Mwamgomo  Meneja wa Benki  ya NMB tawi la Singida mjini, amewapongeza wanasalaam hao kwa moyo wa huruma na kuamua kutoa msaada kama huo na kwamba wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa katika jamii ya Tanzania. Amewaomba waendelee  kuwa na upendo na mshikamano na kusisitiza taasisi nyingine kushiriki katika kutoa misaada kwa watu wanaoihitaji kama walemavu.

Wanasalaam hao nchini wamekutana katika kongamano lao ambalo hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu limefanyika Oktoba 20 Singida mjini.  Katika hafla fupi ya kutoa msaada kwa watoto viziwi, ambayo pia ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini, mwakilishi wa Radio Clouds FM ametoa shilingi laki moja, meneja wa NMB Singida ametoa shilingi laki moja, pamoja na wanasalaam kuchanga shilingi elfu sitini na mbili papo hapo na kufanya jumla ya fedha taslim zilizochangwa kuwa shilingi laki tatu na sitini na mbili elfu.

Shule ya msingi Tumaini viziwi ina jumla ya wanafunzi themanini na mbili, wavulana arobaini na tano na wasichana thelathini na saba. Shule hiyo ina walimu wanane na inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mahudhurio hafifu yanayosababishwa na  baadhi ya wanafunzi kutoka  umbali wa kilomita tisa, upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa, nyumba za walimu na chumba cha kupima usikivu (Audiometry room).  Pia baadhi ya wanafunzi huacha shule kutokana na kuishi mbali na shule.  
Baadhi  ya mikoa iliyowakilishwa na wanasalaam ni Singida, Katavi, Simiyu, Morogoro, Manyara, Arusha, Mbeya

No comments: