Tuesday, October 9, 2012

YALIYONIKUTA MIE NAWEKA HADHARANI


Na. EUFRASIA MATHIAS
Ilikuwa usiku wa ijumaa tarehe14 ya mwezi January 2011 siku ambayo nilipata maumivu kwa kile ambacho nilikifanya kwa nguvu zangu na akili zangu.Chozi ni kitu kilichoko mbali sana na mwonekano wa nje wa mtu lakini pale unapopata maumivu chozi liko karibu kuliko kitu ambacho umekishikilia mkononi mwako
Lilinitoka chozi la huzuni na lenye maumivu makali, nikalia, nikalia, nikatafakari na hatimaye nikahisi nachomwa kisu kwani kile ambacho nilikifanya kwa nguvu zangu na akili zangu hakikuthaminiwa, “aliyefanya hivyo ni sawa na mtu ambaye ananichoma kisu mimi”nilisema
Maumivu niliyoyahisi kwa siku hiyo ni kama yale niliyoyapata asubuhi ya  siku ya jumapili tarehe 31 januari 1999 nilipokuwa napasha maji ya kuoga ili niweze kwenda katika ibada, kwa bahati mbaya maji yamwagika na ule moshi wa moto ukapaa kama ndege ya roketi hadi kwenye kiwiko cha mkono wangu wa kushoto,niliumia sana lakini kwa kuwa ni mvumilivu nilijikaza nilienda kanisani bila kumshirikisha mama yangu kwa maumivu yale niliyoyahisi,
Baada ya kutoka kanisani ndo nikashuhudia kuwa mkono wangu umeumuka kama unga wa ngano ambao umezidishiwa amira, kilichofuata ni kutunmbua ule uvimbe na kuitoa ile ngozi mkononi mwangu,, msomaji wangu maumivu yake……………….
Maumivu hayo ndo nayafananisha na yale alonisababishia mtu ambaye naweza kusema hathamini mwonekano wa mwenzake hasa kwa jamii husika. Mpenzi msomaji, nafikiri umeshawahi kusikia kuhusu mfanyakazi mmoja katika jamii yako ambaye kazi yake yaeza kuijenga jamii au kuibomoa jamii tena kwa sekunde chache kabisa, nisikupe mtihani wa kuwaza mfanyakazi huyo si mwingine ni mwandishi wa habari au mtangazaji.
 Huyu ni mtu ambaye anaaminiwa na jamii na jamii inathamini kazi yake kwa kiwango cha juu kabisa.Msomaji wangu,mfanyakazi huyo akiteleza kidogo tu na kuwaambia jamii jambo Fulani linaloweza kuleta mfarakano baina ya wanajamii, jamii inakuwa katika hali mbaya 
Sekunde moja ni kubwa sana kubadili jinsi mtu alivyo au jambo fulani lilivyo kwani jambo baya husambaa zaidi kuliko jambo zuri,ukifanya mambo kumi mazuri halafu ukafanya jambo baya moja watu watakumbuka na kuliendeleza lile baya moja tu na wakati huo yale yote kumi mazuri hayaonekani tena lakini siku zote waswahili wanasema ukweli hujitenga na ubaya na nuru hung’aa gizani
Sina maana kuwa mimi nilitenda baya moja na mazuri kumi, hapana siko huko kabisa, ninachotaka kukuambia msomaji wangu, kuthamini kitu cha mtu mwingine kama unavyothamini chako ni jambo muhimu sana kwani hilo litadumisha uhusiano mzuri ambao ni nguzo ya amani na maendeleo katika maisha
Kabla sijakueleza kisa chenyewe labda nikudokeze nia ya mimi kukueleza yote haya, chombo cha habari hasa redio kinahitaji sana umakini wa hali ya juu kwani mtangazaji na msikilizaji hawaonani wakati wa mawasiliano kati yao. Kwa hiyo chochote kile ambacho msikilizaji anakisikia au kutokisikia anaamini kimeletwa au kuondolewa na mtangazaji husika. Kwa hiyo mtangazaji anatakiwa autoe ukweli kamili na akiukatisha maana yake si ukweli tena
Msema kweli huwa anajiamini na ana uhakika na kile anachokisema kwa hiyo hana haja ya kukatisha kile ambacho anakitangaza,endapo matangazo yaliyoko hewani yatakatishwa ghafla bila matatzo ya kiufundi inawezekana kuna mashaka ya kile kinachotangazwa. Kwa hiyo kipindi kinapoandaliwa redioni kinatakiwa kisiklizwe na msikilzaji mpaka hitimisho la kipindi lifike
Nisikupeleke mbali msomaji wangu labda nikueleze kilichotokea na kunifanya mimi nilie, nilikuwa naandaa na kukitangaza kipindi katika kituo cha redio fulani ambayo jina lake nalihifadhi, wakati kipindi kiko hewani ( kinasikilizwa) ilikuwa imebaki dakika tatu kipindi kiishe, akatokea mtu mmoja ambaye aliamua kukikatisha kipindi akiamini kuwa kwa muda ule kilitakiwa kianze kipindi kingine, jambo hilo lilifanya msikilizaji alalamike na kuomba kipindi kirudiwe kwani hakufikia hitimisho la kipindi
Aliyekuwa anatangaza ni mimi kwa hiyo msikilizaji anajua kuwa mimi ndo nilimkatishia uhondo aliokuwa akiupata katika kipindi. Kwanini nasema huyo anafanana na mtu anayemchoma kisu mwenzake? Sababu hasa ni kwamba ameniharibia mtazamo wa msikilizaji juu yangu mimi kwani msikilizaji anaamini mimi ndo nimemkatishia uhondo wake wa kukisikiliza kipindi
Kwa ufupi huyu mtu aliyekatisha kipindi  wakati kinasikilizwa  aliniharibia mtizamo wa jamii juu yangu, alimpunguzia msikilzaji imani juu yangu
Thamini,jithamini ili uthaminiwe
 NAKARIBISHA MAONI











No comments: