Thursday, October 11, 2012

MATUMIZI MABAYA YA RASILIMALI ZA UCHUMI

Wakati watanzania tukijinadi bila aibu mbele ya uso wa dunia na kulia bila aibu kuwa SISI NI MASKINI, imebainika kuwa chanzo cha umasikini wetu ni uvivu wa kufikiri, kuamua na kutenda bila kusahau matumizi mabaya ya rasilimali zinazotuzunguka

Si ajabu hata kidogo kuona vijana wakihama kutoka mkoa mmoja kwenda mkoa mwingine wakijikusuru na kujinadi kuwa wanakwenda kusaka maisha na huko hupewa kazi za kulima kwa ujira mdogo huku kwao wakiacha mapori na misitu mikubwa ambayo kama wangeamua kuilima ardhi yake umasikini wangeuaga.

Na kama haitoshi, watanzania tuna tabia ya kudharau na kushindwa kutumia vema zana na vifaa ambavyo vipo au vimeletwa kwa ajili ya kusaidia kukuza uchumi wetu na mwisho wa siku wageni wakija wanauchukua uchumi huohuo mikononi mwetu na kutokomea nao wakituacha na kilio kisicho na mbembelezaji.

Hebu tazama picha hiyo hapo huu, kampuni ya PEPSI imetengeneza masanduku kwa ajili ya kutunzia soda, harafu mtanzania huyu wa mjini SIngida amegeuza masanduku hayo ya SODA kuwa meza ya kuwekea sinki la kunawia wateja katika mgahawa wake

JE KWELI WATANZANIA TUKO MAKINI NA SUALA LA KUPAMBANA NA UMASKINI? mimi sijui na sina jibu la swahi hili, Hebu tujadili pamoja, lete MAONI

No comments: