Thursday, October 4, 2012

SHEKHE WA MKOA WA DODOMA AONGOZA SALA KUIOMBEA STANDARD RADIO



EUFRSIA MATHIA

Shehe mkuu wa Mkoa wa Dodoma  Mustapher Shabaan ametembelea Kituo cha Standard Radio Fm 90.1 Mhz Singida  na kuendesha sala maalumu ya kuiombea Radio hiyo ili itumike kukuza ustawi na maendeleo ya watanzania sambamba na kuhamasisha jamii kuepuka udini na kujanga maelewano miongoni mwa watanzania.
Ziara ya Shehe Shaaban iilitokana na furaha yake ya kusikia ujio wa radio ya kwanza naya pekee mkoani Singida ambao haukuwahi kuwa na radio kabla.
Sshekhe Mstapher Shaaban katika ofisi za Standard Radio FM mjini Singida

Ujio wa radio mkoani Singida ulimpa imani kuwa jamii nzima itapata elimu ya dini ikiwa ni sehemu ya maisha binadamu 
Shehe huyo aliiombea radio hiyo iweze kupata mafanikio katika shughuli zake kwani radio imeletwa kwa nia ya kusaidia wananchi wote hasa wale wasiosikika kama moto wa radio unavyosemea  “Naiombea Baraka radio hii kwa Allah kwani radio itakuwa mkombozi wa watu wasiosikika” alisema shehe huyo
Shekhe Shaaban akiwa na  viongozi wa dini ya kiislamu mkoani Singida wakiwa katika ofisi za Standard Radio fm

Hi ni mara ya kwanza kwa viongozi wa juu ya dini kuitembelea Radio hii ingawa vikundi mbalimbali vya wana dini za kikristo wamekuwa wakifika kuona kituo hiki,
Tunatumia fursa hii kuwaalika viongozi wa dini zote kututembelea na kutupa maoni mbalimbali ikiwemo kuuliza maswali na hata kutuletea kazi zao za uinjilishaji hususani Qaswida na kwaya za injili.

No comments: