Tuesday, October 23, 2012

POLISI WASHIRIKI MAHAFALI SHULE YA MSINGI

Baadhi ya wanafunzi wakifuahia jambo wakiwa pamoja na mtoto wa rais Kikwete Ndg. Ridhiwani. Picha na mtandao wa google.
 
Na Daud Nkuki
Singida Oct 23, 2012
Wazazi na walezi wamekumbushwa kuzingatia wajibu na majukumu yao ya kuwalea na kuwaendeleza watoto wa kielimu.
Mkuu wa kituo cha Polisi Mtinko, wilaya ya Singida vijijini, Inspekta Iledefonce Bernard Kagaruki, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliyasema hayo katika sherehe za mahafali ya 35 katika shule ya msingi Malolo wilayani humo.
Inspecta Kagaruki amewaangaliza kuhusu umri mdogo wa kumaliza elimu ya msingi ambao ni kati ya miaka 12 na 14, hautawasaidia wazazi katika shughuli za kimaendeleo ambazo huhitaji zaidi nguvu kazi, wanaporudi kijijini.
Ameendelea kuwaasa wasiridhike na kiwango cha elimu hii bali iwe ni kichocheo cha kuendelea na elimu ya juu ya sekondari wala wasiwe na tamaa ya kuwaoza au kuswaga ng’ombe huko porini.
“Watoto watakaofanyiwa vitendo hivyo, waripoti polisi ili sheria ichukue mkondo wake” aliagiza.
Kusoma sio lazima kuajiriwa, kwa elimu hiyo kile watakachokifanya hakina budi kibadilishe maisha yao na ya wazazi wao.
Uwezo wa kushiriki vyema na kuzingatia elimu wanayopewa watoto ni pamoja na kupatiwa chakula cha mchana ambacho hakina budi kuwekewa mkazo na wazazi ama walezi.
Aidha wale wenye dhamana ya kutunza mifuko ya chakula cha wanafunzi, wawe waaminifu kulingana na mahitaji ya watoto.
Jumla ya wanafunzi 112 kati ya 176 wakiwemo wasichana 63 na wavulana 49 wamehitimu elimu ya msingi shuleni hapo .
Mwisho

No comments: