Wednesday, October 17, 2012

VITUKO VYA KAZI NI UBUNIFU, UMAKINI NA MAANDALIZI

Mfanyakazi wa aina yoyote hulenga kufikia malengo bila kuwa na athari katika eneo lake, na maandalizi ndiyo njia pekee inayomwezesha mfanyakazi yeyote kufikia malengo yake.
Wakati mwingine tunalazimika kufanya kazi katika amazingira magumu lengo tu ni kuhakikisha tunafanikisha tuliyopanga kama malengo yetu ya simu
Angalia picha katika ukurasa huu juu na chini, hawa ni watu makini walioko katika malego na harakati za kuyafikia
Hapa wanajiandaa kuingia katika moja ya ofisi za umma, hivyo wanajiweka sawa kabla kwa kuweka safi nywele, hii ina maana kuwa unadhifu ni muhimu sana uingiapo katika ofisi yoyote
PICHA YA PILI

Huyo ni mwanahabari makini bila kujali kuwa hapa ni barabarani na kwamba inaweza kutokea gari au chombo chochote cha usafiri anachukua pozi na kupiga picha ya tukio muhimu, kweli uandishi wa habari hasa za picha ni wito, wengine wanalala hadi chini au kujificha vichakani ili kupata picha nzuri, si unajua tena baadhi ya wanene (boss) hawataki kupigwa picha au miradi yao kuonekana. Pig up dada
PICHA YA 3 -MASIKITIKO
Watu wengi hushindwa kutofautisha muonekano wao na mazingira waliyomo, hii imekuwa kama ni jambo la kawaida kabisa katika jamii yetu. si ajabu kwa mtanzania kuvaa nguo ya ofisini akiwa disko, wengine wanavaa mavazi ya kuogelea wakiwa vyuoni au hata ofisini, wala huoni hatari kumuona binadamu akivaa chupi na sidiria pekee awapoo barabarani au hata katika kumbi za starehe na burudani, mbaya zaidi hushangai kumuona jamaa yako akicheka na kutabasamu penye majonzi na masikitiko. Kwa wanahabari hawa wa kampuni ya STANDARD VOICE LTD hali ni tofauti, wawapo ofisini, wawapo mtaani maeneo ya raha, maeneo ya matatizo na maeneo ya kazi za uandishi wao wanafanana na mazingira hayohayo
Wafanyakazi wa standard Radio fm, wakiwa msibani katika kijiji cha Mwankoko Singida ambako mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alitekwa na kukatwa mkono kwa imani za kishirikina na kisha kuuwawa kwa kuchomwa moto.
Picha zote na Prosper Kwigize SRfm

No comments: