Tuesday, October 2, 2012

TANESCO SINGIDA YAOMBA USHIRIKIANO



Na,Doris Meghji
Singida

Shirika la ugavi nchini (TANESCO) limewataka wananchi wa mkoa wa Singida kuipokea miradi ikiwa  ni pamoja na kutumia fursa kuunganishwa na huduma ya umeme kwenye miradi hiyo inayopita katika maeneo yao ndani ya muda wa miradi kutekelezwa lengo likiwa ni kumpunguzia gharama mteja za kuunganishwa na huduma hiyo ya umeme.

Meneja wa Tanesco Mkoa wa Singida Bwana Maclean Mbonile amesema hayo kwa waandishi wa habari mkoa wa singida kwa kuomba ushrikiano nao kupitia vyombo wanavyofanyia kazi kwa kuelimisha wananchi kutumia fursa hizo.

Meneja huyo ameomba waandishi wa habari kuhamasisha wananchi kupokea miradi hiyo ya umeme inayotekelezwa katika maeneo yao,kuwa tayari kuunganisha na huduma hiyo ya umeme ndani ya muda wa mradi kutekelezwa kwa gharama nafuu ikiwa ni pamoja na kuwa walinzi wa miundo mbinu ya umeme katika miradi hiyo.

Hata hivyo jumla ya miradi minne ya umeme chini ya ufadhili wa wakala wa nishati vijijini (REA) kupitia msimamizi mkuu Tanesco inatekelezwa mkoani singida ambayo ni mradi wa Manyoni – Kilimatinde  na Mradi wa Itigi Mgandu yenye kugharimu kiasi cha shilling billion 7 iliyoanza Julai 2010 inatarajiwa kukamilika Disemba mwaka huu.

Wakati mradi wa Mandewa – Sepuka wenye urefu wa kilomita 25 utakao tumia transfoma 8 na mradi wa wilaya mpya wa Mkalama wenye urefu wa kilomita 173 utakao tumia transfoma 17 inatarajiwa kugharimu kiasi cha shilling billion 18,300,000,000/= zitatumika kukamilisha miradi hiyo kwa kipindi cha miezi 13.

Hadi sasa jumla ya wananchi 28,380 wameunganishwa na huduma ya umeme  katika manispaa ya Singida ambao ni sawa na asilimia 16 ya wakazi 153,000 ya idadi ya watu kwa mujibu wa sensa ya watu mwaka 2008.



No comments: