Thursday, October 18, 2012

RPC SINGIDA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI

Na, Khadija Mahamba 

Singida
Kufuatia kuwepo kwa vurugu za kidini nchini Tanzania zilizopelekea kuchomwa kwa makanisa kadhaa nchini, jeshi la polisi mkoani singida linafanya mazungumzo na viongozi wa dini kwa lengo la kutafakari hali hiyo na kutafuta ufumbuzi wa hali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa singida Kamishna msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa leo amekutana na viongozi wa dini ya kikristo mkoani humo huku akiahidi kukutana tena na viongozi wa dini ya kiislamu ijumaa October 19, 2012
Aidha katika mipango ya jeshi hilo, kamanda Sinzumwa October 22 mwaka huu, anatarajia kuwakutanisha viongozi wa dini zote mbili wakristo na waislamu kwa lengo la kujadiliana kuhusu namna ya kumaliza tofautii zao na kukomesha vurugu za kidini nchini.
Hata hivyo kamanda Sinzumwa amekataa kueleza mazungumzo hayo yalivyokuwa kwa madai kuwa umakini unahitajika kabla ya kuyatangaza mazungumzo yao na kwamba atafanya hivyo baada ya kukutana na pande zote mbili.

No comments: