Tuesday, October 2, 2012

MGOGORO WA MACHIMBO YA MADINI SINGIDA


NA  Phesthow  Sanga  
Iramba
Viongozi  17 Wakiongozwa  na Diwani  Wa  Kata  ya  Ntwike  Mhe, Albart  Makwala , Mwenyekiti  wa Serikali  ya  Kijiji cha  Nkonkilangi,  Tano  Mussau , Ofisa Tarafa,  Luther Mpndu  Pamoja  na Wajumbe Wa Halmashauri  ya kijiji  hicho  na Wazee  Maarufu  wa  kijiji,  katika  Tarafa  ya Shelui  Wilayani  Iramba  Waliandamana kwa  Mkuu wa  Wilaya  kutaka kujua  Hatma  ya Mgodi Wao.
Hatua hiyo Imejiri  Baada  ya siku  mbili  tu ya kupigwa  Stop  kwa  mgodi  huo  kufanya kazi na Mahakama septemba 27 mpaka Maamuzi ya kesi mama Itakapotoa  Uamuzi wa mmiliki Halali wa machimbo hayo .
Viongozi  hao waliofika  kwa  Mkuu  wa  Wilaya ya Iramba  Yahya  Ismail Nawanda na kumweleza kuwa  Baada ya Mahakama kutoa  Amri  ya kusimamishwa  kwa  Shughuli  Za  Mgodi   Mbele  ya  Kiongozi  Wao wa  Mgodi,  na Anayesimamia  Kesi yao  dhidi  ya John Bina,  pamoja na kuitii  Amri hiyo Lakini  John  Bina  Amekiuka  Amri  halali ya  Mahakama  kwa  Kuvamia Mgodi na kufanya Uharibifu  wa  Mali.
Diwani  Albert Mkwala  Pamoja  na Viongozi Wengine Walimpa DC huyo  Malalamiko  kuwa  John Bina  na  Wenzake wametia  Chumvi  Kwenye  Mashine  Nne  za  Kuvuta  Maji  Zenye  Ukubwa  wa  Vlt 24 aina ya  AMEC, kutoka  China  Zenye  Thamamani  ya  Shilingi  milioni  Nane   na Laki  Nane {8.800.000.}
Aidha  Wameeleza  kuwa  Ndani  Ya  Mgodi wao  Kuna  Jumla ya  Duara Ishirini Na  Moja  lakini  kutokana  na  kuwekwa   Chumvi  kwenye  Mashine  Za  kupampu  Maji  Tayari  Duara Tatu Zimetumbukia  nyeye dhamani  ya  Milioni  Mia Tatu   ambazo  Zilishaanza  kutoa  Madini  Na  kuanza  kulipa  gharama za Uchimbaji  kwa  Wenye  Maduara  hayo .
Viongozi  hao  wamesema   kuwa  Mpaka   Sasa  Kuna  Waathirika Elfu Moja  wa  kiuchumi  ambao  hutegemea  Machimbo  hayo baada  ya kusimama kuchimba  Madini na kujipatia kipato ,”Wamesema kuwa , Licha ya hilo  kuna  Wananchi  Elfu  Tano  Ambao Wameathirika  Kiuchumi  pia kupitia kusimamishwa  kwa  Machimbo  hayo.” Wamekazia .
Diwani Albert  Amesema  kuwa  Walipofika  kwa DC  Nawanda,   hakuwa  Tayari  kuwasikiliza  kinyume chake Alinza  kuwatukana   na  kuwa kemea  huku  Akitishia  kumweka  ndani Emmanuel  Magai na  Kumwita  Magai  kuwa  ni  Mjinga  kwanini  hataki  kuweka  Mkataba   na  John Bina.
 Hata hivyo watu  hao  wamedai  kuwa  Wao  Walitii  Mamlaka  ya  Mahakama  tu kwani  leseni  Ya  Bina Inasoma ni ya kijiji Cha Mgongo  na Siyo  Nkonkilangi Ambayo ndiko Ugomvi  Upo na Kudai huo ni Uone vu  Fulani, na Kuiomba Serikali Kuingilia kati  Kusuluhisha  Mgogoro huo  mapema .
Juhudi  za  kumtafuta  John  Bina  na  Wenzake  Kwa  Njia  Simu,  Kuzungumzia  Tuhuma Zinazo Mkabili  Za  kuweka   Chumvi  kwenye  Mashine  Za  kupampu Maji  kwenye  Mashimo  ya  Maduara  zimegonga  Mwamba  kwa  kukataa  Kupokea Simu  ilipokuwa inaita mpaka inakatika  bila majibu.
                                                 


No comments: