Thursday, October 18, 2012

WAWILI WAFA KWA AJALI SINGIDA.


Na Edilitruda Chami na Abduli Bandola
Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali mbili tofauti mkoani Singida,  ikiwemo ya mtu mmoja kugongwa na  gari na mtu mwingine  kuanguka kwa pikipiki iliyokuwa katika mwendo kasi  na kusababisha  kifo.
Akizungumza  na Standard Radio Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa  amesema kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mussa (23),  amegongwa na kufa papo hapo na gari lenye namba za usajili T 887 BFS aina ya Scania, mali ya Benevoti Jovin likiendeshwa na Shaban Abbas  lililokuwa likitoka Dar-es-salaam kuelekea Nzega . Ajali hiyo imetokea maeneo ya kibaoni manispaa ya Singida Oktoba 16, 2012.
Amelitaja tukio la pili kuwa  ni  la dereva wa pikipiki yenye namba za usajili T 278 BAH  aina ya LUG SUN aliyefahamika kwa jina la Mustafa  Museko kufa papo hapo baada ya kuwa katika mwendo kasi  na kusababisha ajali iliyomsababishia mauti. Amesema  pikipiki iligonga mti katika kijiji cha Malima wilaya ya Ikungi  usiku wa kuamkia terehe 18 Oktoba  2012.
Kamanda Sinzumwa ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika utumiaji wa alama za barabarani na kupunguza mwendo kasi ili kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea siku hadi siku.

No comments: