Wednesday, October 16, 2013

RAIS JAKAYA AKUTANA NA VYAMA SITA VYA SIASA JIJINI DAR ES SALAAM




 
Na.Mwandishi wetu

rais jakaya kikwete jana amekutanana na viongozi wa vyama sita vya siasa, vyenye uwakilishi bungeni, ikulu, jijini dar es salaam na kukubaliana mambo makuu mawili.

rais kikwete  amekubaliana na vyama vyote vya siasa vyenye mawazo, maoni na mapendekezo ya kuboresha muswada wa sheria ya marekebisho ya sheria ya mabadiliko ya katiba wa mwaka 2013, kuyawasilisha haraka serikalini, ili kutafuta namna ya kuyashirikisha katika marekebisho ya sheria hiyo.

aidha amesema vyama vya siasa nchini, kama wadau muhimu katika mchakato wa katiba mpya, viangalie namna ya kukutana na kujenga mfumo wa mawasiliano na maridhiano, wa jinsi vitakavyosukuma mbele mchakato mabadiliko ya katiba ya nchi, kwa maslahi mapana ya nchi na mustakabali wa taifa.

katika makubaliano hayo, kituo cha demokrasia tanzania (tcd), kimepewa jukumu la kuratibu jambo hilo, ikiwa ni pamoja na kuandaa mkutano wa vyama hivyo na wadau wengine nchini.

No comments: