Wednesday, October 16, 2013

FAMILIA YANUSURIKA KIFO BAADA YA KIMBUNGA KUEZUA NYUMBA MKOANI SINGIDA


Na.Hawa Mkhandi
familia moja imenusurika kufa kufuatia kimbunga kuezua nyumba wanamoishi ,katika wilaya ya ikungi mkoani singida

 
tukio hilo limetokea jana majira ya saa kumi na nusu jioni, katika kijiji cha choda kata ya mkiwa tarafa ya ikungi

 
akizungumza na standard redio diawani wa kata ya mkiwa bw mathias sungita, ametaja walionusurika kuwa ni familia ya  bw saimon joram

 
imelezwa kuwa upepo mkali uliofuatana na kimbunga ulizingira nyumba ya bw sungita, na kuezua paa wakati familia hiyo ikiwa ndani

 
wananchi wametakiwa kutoa msaada kwa familia hiyo ambayo kwa sasa haina sehemu ya kuishi
 

No comments: