Na Edilitruda Chami na Abduli Bandola
Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali mbili tofauti mkoani Singida, ikiwemo ya mtu mmoja kugongwa na gari na mtu mwingine kuanguka kwa pikipiki iliyokuwa katika mwendo kasi na kusababisha kifo.
Akizungumza na Standard Radio Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa amesema kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mussa (23), amegongwa na kufa papo hapo na gari lenye namba za usajili T 887 BFS aina ya Scania, mali ya Benevoti Jovin likiendeshwa na Shaban Abbas lililokuwa likitoka Dar-es-salaam kuelekea Nzega . Ajali hiyo imetokea maeneo ya kibaoni manispaa ya Singida Oktoba 16, 2012.
Amelitaja tukio la pili kuwa ni la dereva wa pikipiki yenye namba za usajili T 278 BAH aina ya LUG SUN aliyefahamika kwa jina la Mustafa Museko kufa papo hapo baada ya kuwa katika mwendo kasi na kusababisha ajali iliyomsababishia mauti. Amesema pikipiki iligonga mti katika kijiji cha Malima wilaya ya Ikungi usiku wa kuamkia terehe 18 Oktoba 2012.
Kamanda Sinzumwa ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika utumiaji wa alama za barabarani na kupunguza mwendo kasi ili kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea siku hadi siku.
No comments:
Post a Comment