Wakazi wa eneo la Ginnery Kata ya Mandewa manispaa ya Singida, wakiwa wamekusanyika katika moja ya gati la maji kupata huduma hiyo.
Na Abdul Bandola.
Mkoa wa Singida unakabiliwa na tatizo la uhaba mkubwa wa maji ambalo limefanya baadhi ya watu kuacha kufanya shughuli za maendeleo na kulazimika kutembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi kutafuta maji.
Hali hiyo inatokana na kuchelewa kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji unaojengwa katika kijiji cha Mwankoko katika manispaa ya Singida chini kampuni ya Spencon ya nchini India, ulitarajiwa kukamilika mwezi April mwaka 2012 lakini hadi sasa bado haujakamilika.
Akizungumza na Standard Radio ofisini kwake, Meneja wa Mamlaka ya maji manispaa ya Singida SUWASA Mhandisi Kombe Mushi, amesema mkandarasi wa mradi huo ameahidi kukabidhi Desemba 31, 2012.
Aidha mhandisi Mushi anaunga mkono ucheleweshaji huo huku akitaja kuwa ucheleweshaji huo umetokana na kucheleweshwa kwa pampu za maji ambazo zinashikiliwa bandarini Dar es salaam na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa madai kuwa hazijalipiwa kodi.
Hata hivyo uchunguzi wa standard blog umebaini kuwa madai hayo na lawama dhidi ya TRA ni matokeo ya mipango mibovu ya Halmashauri kwani miradi ya jamii zana zake kuondolewa kodi baada ya rasimu ya mradi na mapendekezo ya vifaa kuwasilishwa TRA kuombewa kuondolewa kodi.
eneo la chanzo cha maji Mwankoko kikiendelea kujengwa, wanaoonekana ni mafunzi wa TANESCO wakifunga mtambo wa umeme. picha zote na Doris Meghji
Hadi sasa mradi huo umegharimu shilingi bilion 23 na yapoo mashaka kuwa ahadi ya kukamilika mwezi desemba ni ya kufikirika kulingana na kasi ya ujenzi wake
No comments:
Post a Comment