Friday, October 12, 2012

TANESCO SINGIDA YALIPA FIDIA WANANCHI

Na. Elsante John
Singida

HALMASHAURI ya Wilaya Singida imepokea zaidi ya Sh. Bilioni Mbili, kutoka TANESCO kwa ajili ya fidia ya wananchi kupisha umeme gridi ya Taifa, kutoka Iringa kwenda mkoani Shinyanga.
 
Mwenyekiti wa halmashauri hiyo Celestine Yunde amesema tayari zaidi ya Sh. Milioni 299.9 zimelipwa kwa wananchi 45, waliofungua akaunti katika benki ya NMB, CRDB na NBC.
 
Amesema kiasi kingine cha fedha taslimu zaidi ya Sh.Milioni 277 kimelipwa kwa wananchi 387, wakati kiasi kingine cha zaidi ya Sh. Milioni 891.1 kipo tayari kwa malipo ya awamu ya pili kwa wanachi 128, kupitia kwenye akaunti zao 
 
Akichangia hoja hiyo, mbunge wa Singida mashariki Tundu Lisu amesema zoezi hilo limewapunja wananchi, na hivyo kwenda kinyume na sheria ya ardhi ya mwaka 2001

No comments: