NA Phesthow sanga
Ajali mbaya iliyotokea Usiku wa Kuamkia oct 03 Mwaka huu katika Kijiji Cha Malendi Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Mkoani Singida na kuwa Watu watatu.
Watu Waliofariki Dunia papo hapo Walifahamika kuwa ni Suleiman Kaberege { 21} Mhehe Mkazi Wa Igunga Mkoani Tabora Wengine ni Mwanamke aliyefahamika Kwa jina moja la Mwanaid Pamoja na Mtoto Wake Ambaye hakuweza Kufahamiaka jina mara moja.
Akiongea na Wanahabari Katika Hospitali ya Wilaya ya Iramba jana Matron wa hospitali hiyo Bi ,Perpetua Mnkumbo alisema Kuwa, Usiku wa saa sita kuamkia Oct 3 walipokea miili ya marehemu Watatu na Majeruhi Ishirini na saba 27 na Baadaye wawili Walifariki Dunia wakati madaktari na manesi wakiendelea kuwahudumia.
Aidha Aliwataja Waliofariki Hospitalini hapo kuwa ni Pamoja na Nana kulwa{ 16} na Erasto Willimu {39},alisema kuwa Majeruhi Wengine Waliweza Kupewa Rufaa ya kwenda Hospitali kubwa kwa Matibabu Zaidi, Kutokana na kuendelea kutoka damu mdomoni.
Akielezea Chanzo Cha ajali hiyo Jumapili Elia{ 43} Ambaye ni Mhanga wa Ajali Alisema kuwa Gari hilo halikuwa na Taa
Kutokana na kukithiri kwa Ajali Nyingi Barabarani Wananchi Walioshuhudia Ajali hiyo Mbaya Wamelishauri Jeshi la Polisi Nchini Hasa Askari wa Usalama Barabarani kuwa Makini na Madereva Wazembe na wasiozingatia Sheria za barabarani, Polisi Wilayani hapa Wamethibitisha Kutokea Kwa Ajali hiyo na juhudi za Kumutafuta Dereva Wa gari hilo Zinaendelea .
Jeshi la polisi mkoani Singida limekiri kutokea kwa ajali hiyo
No comments:
Post a Comment