Thursday, October 11, 2012

RC SINGIDA AONYA UHARIBIFU NA MATUMIZI MABAYA YA BARABARA

Moja ya barabara zinazojengwa nchini Tanzania ambazo hata hivyo zinatajwa kuharibiwa na wananchi ambao ama huvunja kingo za madaraja, kuiba alama za barabarani au kuchimba mashimo kwa nia ya kusababisha ajali. Picha na. Prosper Kwigize

Na: Abdul Bandola.
Mkuu wa  mkoa  wa Singida Dk. Parseko Kone amewaasa wananchi wa mkoa wa  singida kuwa na matumizi mazuri ya barabara ya kiwango cha lami inayounganisha mikoa ya Singida na Arusha baada ya baadhi yao kuitumia vibaya barabara hiyo.
Dk. Kone amesema hayo  wakati wa ziara yake na meneja wa TAN ROADS mkoa wa Singida Bw. Yustas Kangole iliyofanyika tarehe 10 october 2012, kutembelea vijiji vya singida vilivyoko kando kando mwa  barabara hiyo.

Mkuu wa Mkoa wa Singida Dr. Paraseko Kone katika shughuli za ukaguzi wa miradi mkoani humo.

Mkuu huyo wa mkoa wa Singida  Dk. Kone amesema kuwa kuna baadhi ya wananchi wanaoweza kubomoa barabara ya lami kwa kutumia sururu na kuiba alama za barabarani ,na kuongeza kuwa watakaobainika kufanya vitendo hivyo vya uharibifu hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi yao.
Aidha, Dk.  Kone ameongeza kusema kuwa wakazi wa kijiji cha  Kisasida wilaya ya Singida mjini pamoja na vijiji jirani,  wanaendelea kunufaika na mradi wa maji uliopo maeneo hayo kwa kupata maji ya kutumia na hata kwa mifugo yao. Mradi huo wa maji ulijengwa ili kurahisisha shughuli za ujenzi wa barabara hiyo.

No comments: