Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makni kumsikiliza mwezeshaji katika mafunzo
ya sera na ufuatilaji wa bajeti ukumbi wa social training centre
manispaa ya singida
NA,
Doris Meghji
Singida
Elimu
ndogo ya uchambuzi wa sera miongoni wa waandishi wa habari nchini ni sababu kuu
mojawapo inanyopelekea kutohabarisha umma juu ya mambo mbali mbali ya maendeleo
imefahamika.
Hayo
yamebainika leo mkoani Singida kwa waandishi wa habari mkoa wa singida katika
mafunzo uchambuzi wa sera na ufuatiliaji wa bajeti(policy analysis and budget
tracking) yaliyoandaliwa na Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari
Tanzania(UTPC) kwa waandishi wa habari wa mkoa huu.
Akiongea
na Standard Radio Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Adam Ndokeji toka mwanza
amewataka waandishi wa habari kubadilika kwa kufanya uchambuzi wa sera mbali
mbali za masuala ya maendeleo lengo likiwa ni kuuhabarisha umma kwa mambo ya
kimaendeleo.
Naye
mmoja wa waandishi wa habari wa mkoa wa singida Bi Awila Silla anasema
“nimefurahia sana mafunzo hayo ingawa yamechelewa kujifunza kwani tayari
tulishavirunda kuripoti mambo mengi ya maendeleo katika umakini na umahususi
unaotakiwa,hata hivyo ni wakati muufaka sasa wa mtazamo chanya kuahidi kuwa
elimu ya mafunzo haya itaondoa mapungufu yote ya nyuma”amesisitiza Bi
silla.
Katika
mafunzo hayo jumla ya waandishi kumi na nane(18) wanapatiwa mafunzo hayo mkoani
singida yatakayodumu kwa kipindi cha siku nne.
No comments:
Post a Comment