Ama kweli maji ni
uhai
Na Eufrasia Mathias
Ikiwa imebaki muda usiopungua miezi miwili kukamilka kwa
mradi wa maji mkoani Singida bado hali ya maji inazidi kuwa tete kiasi kwamba
watu wanatamani kuhamia maeneo ambapo kuna visima na mabomba yanayowategemeza
watu wa maeneo husika ili tu waweze
kuwahi foleni ambayo hutokea na kufurika maeneo hayo wakati maji yanapoanza kutoka
Kwa ujibu wa Meneja wa Mamlaka ya maji manispaa ya Singida SUWASA
Mhandisi Kombe Mushi, mkandarasi wa
mradi wa maji unaojengwa anatarajiwa
kukabidhi mradi huo Desemba 31, 2012. Kwa hali halisi ilyopo eneo la ujenzi huo
sina uhakika kama miezi miwili itatosha kukamilisha ujenzi huo
Ukitazama mabomba yaliyoko nje ya eneo la ujenzi ambayo
yanatakiwa yatumike kukamilisha mradi huo unaweza kukadiria muda mrefu zaidi
unahitajika kukamilisha mradi huo. Swali ni kwamba mradi unajengwa, wakazi wa
Singida watateseka mpaka lini?
Inashangaza kuona mtoto mdogo kazidiwa na kiu hadi anataka
kutumbukia katika dumu tupu lililopo kwenye foeni inaosubiri maji yatoke baada
ya muda usiojulikana. Jamani tuwe na mawazo mapana
No comments:
Post a Comment