Na edilitruda chami
Mkoa wa shinyanga umeendelea kushamiri katika mashindano ya mbio za baiskeli ambapo chama cha wapanda biskeli katika wilaya ya shinyanga vijijini {CHABASHI} kimeweza kuandaa mashindano ya umbali wa kilomita 35 kutoka kijiji cha Itwangi kwenda Puni kwa kilomita 20 na kutoka itwang kwenda kituli kwa kilomita 15 ambapo washiriki 26 walijitokeza katika mbio hizo.
Juma Tagara ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza, na akazawadiwa taslim sh. laki moja akifuatiwa na masingija ndumrli ayeliweza kuibuka na taslim shilingi elfu sabini na mshindi wa tatu alikuwa ni Charles Clement aliejinyakulia kitita cha sh. elfu hamsini zilizotolewa na mdhamini wa mbio hizo Senge Sesaguli.
Katibu wa chama cha mbio za Baiskeli wilaya ya shinyanga vijijini Shija Dalali amesema kuwa lengo la kugawa zawadi hizo kwa washindi katika mashindano hayo ni kuhamasisha vijana kushiriki katika mashindano mbalimbali na kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji vya wanamichezo watakaoshiriki katika ligi mbali mbali. vijijini
Mbali na mbio za baiskeli mkoa huo unaendesha mashindano mbalimbali ambapo zawadi za vitu halisi hutolewa kama vile ngombe mnyama, mbuzi mnyama, mpira wa miguu na pamoja na fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na wadhamini mbalimbali.
No comments:
Post a Comment