Tuesday, October 23, 2012

MKE AUWAWA KWA WIVU WA MAPENZI

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida ACP Linus SInzumwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake
 NA. HALIMA JAMAL
Singida  MCHIMBAJI mdogo wa madini mkazi wa kijiji cha London wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Joshua Lazaro (46),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumuuwa mke wake Tatu Mathias(46) kwa madai kuwa anatembea nje ya ndoa. Akizungumza na waandishi wa habari juzi jioni ofisini kwake, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa,alisema tukio hilo la kusikitisha,limetokea oktoba 21 mwaka huu majira ya jioni. Alisema mauaji yaho yamechangiwa na wivu wa mapenzi uliopitiliza ambapo Joshua alikuwa anamhisi mke wake Tatu,anatembea nje ya ndoa. Sinzumwa alisema mtuhumiwa Joshua alimchoma mke wake tumboni na chuma na kusababsiha utumbo wote kumwagika nje na kusababisha kifo cha Tatu papo hapo.Mtuhumiwa Joshua alikamatwa muda mfupi baada ya kufanya mauaji hayo. Kamanda huyo alisema upelelezi utakapokamilika,mtuhumiwa Joshua atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Katika tukio jingine,Sinzumwa alisema lori aina ya Volvo T.210 CDZ lililokuwa linavuta tela T.964 CBV,limeteketea kwa moto na tela lake, baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme. Alisema tukio hilo limetokea oktoba 21 mwaka huu, saa tisa alasiri katika barabara kuu ya Singida- Mwanza katika eneo la kijiji cha Nkwae wilaya ya Singida. “Pamoja na lori hilo na tela lake kuteketea kwa moto,pia mitumba mbalimbali na shehena ya viatu vilivyokuwa vinasafirishwa kutoka Dar-es-salaam kupelekwa jijini Mwanza,navyo vimeteketea.Ni mitumba na viatu vichache vimeokolewa.Hadi sasa bado hatujafahamu thamani ya uharibifu huo mkumbwa”alisema. Kamanda Sinzumwa alisema lori hilo siku ya tukio,lilikuwa likiendeshwa na Daud Kanoni Mwakatobe (36) mkazi wa jijini Mbeya.Uchunguzi zaidi kuhusiana na moto huo,bado unaendelea.

No comments: