Wednesday, October 17, 2012

MSINDAI AIBUKA KIDEDEA CCM SINGIDA

Mgana Msindai mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida

Na. Doris Meghji
Mgana Izumbe Msindai ameibuka kuwa mshindi katika uchaguzi wa uenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Singida  mkoa  jana uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Utumishi wa Umma manispaa ya Singida

Waliogombea nafasi hiyo ya mwenyekiti ni Bw. Jorum Sima Alute aliyepata kura 194, Amani Andrew Rai aliyepata kura 238 na Mgana Izumbe Msindai aliyepata kura 407 kati ya kura  837 zilizopigwa  na kuufanya uchaguzi urudiwe ambapo Mgana Msindai alipata kura 673  na Amani Rai alipata kura 41 kati ya kura halali 714 


No comments: