Na. Boniface
Mpagape.
Chama cha
watuma salaam kupitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini, kimetoa msaada
kwa watoto viziwi wanaosoma katika shule ya msingi
Tumaini iliyopo katika manispaa ya Singida.
Watuma
salaam hao nchini wametoa msaada wa vitu
mbali mbali vikiwemo sabuni, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi na fedha taslim
shilingi laki moja.
Katika risala yao watuma salaam hao nchini
wamesema ni vyema pia kwa taasisi
nyingine na watu wenye mapenzi mema nchini kuiga mfano wa kutoa misaada kwa watu
wenye mahitaji na kutoiachia jukumu hilo serikali pekee. Wamesema misaada kama hiyo imetolewa pia
katika mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Mbeya, Morogoro, Manyara, na
Dodoma. Aidha wametoa wito kwa jamiii kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI.
Mgeni rasmi
katika hafla hiyo, Bi. Christina Mwamgomo Meneja wa Benki ya NMB tawi la Singida mjini, amewapongeza
wanasalaam hao kwa moyo wa huruma na kuamua kutoa msaada kama huo na kwamba
wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa katika jamii ya Tanzania. Amewaomba
waendelee kuwa na upendo na mshikamano
na kusisitiza taasisi nyingine kushiriki katika kutoa misaada kwa watu
wanaoihitaji kama walemavu.
Wanasalaam
hao nchini wamekutana katika kongamano lao ambalo hufanyika kila mwaka, ambapo
mwaka huu limefanyika Oktoba 20 Singida mjini.
Katika hafla fupi ya kutoa msaada kwa watoto viziwi, ambayo pia
ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini,
mwakilishi wa Radio Clouds FM ametoa shilingi laki moja, meneja wa NMB Singida
ametoa shilingi laki moja, pamoja na wanasalaam kuchanga shilingi elfu sitini
na mbili papo hapo na kufanya jumla ya fedha taslim zilizochangwa kuwa shilingi
laki tatu na sitini na mbili elfu.
Shule ya
msingi Tumaini viziwi ina jumla ya wanafunzi themanini na mbili, wavulana
arobaini na tano na wasichana thelathini na saba. Shule hiyo ina walimu wanane
na inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mahudhurio hafifu
yanayosababishwa na baadhi ya wanafunzi
kutoka umbali wa kilomita tisa, upungufu
wa vyumba vitatu vya madarasa, nyumba za walimu na chumba cha kupima usikivu
(Audiometry room). Pia baadhi ya
wanafunzi huacha shule kutokana na kuishi mbali na shule.
Baadhi ya
mikoa iliyowakilishwa na wanasalaam ni Singida, Katavi, Simiyu, Morogoro,
Manyara, Arusha, Mbeya
No comments:
Post a Comment