Tuesday, October 9, 2012

MAGUFULI AITEMEA CHECHE KAMPUNI YA UJENZI YA CHICO



Waziri Magufuli na msafara wake wakikagua barabara eneo la Sekenke -Sherui inayotakiwa kurudiwa kutokana na kutokidhi viwango, Kampuni ya Chico imeshinikizwa kurudia ujenzi huo.
Na, Doris Meghji 
Singida
Waziri wa wizara ya Ujenzi Dr. John Pombe Magufuli amezitaka kampuni za wakandarasi wanaojenga barabara nchini kujenga barabara kwa viwango na kuzingatia uthamani wa fedha (value for Money) ili kuepuka adhabu za kurudia kazi na kutopewa zabuni za ujenzi wa barabara nchini.

Dr.Magufuli ametoa kauli hiyo leo mkoani Singida alipotembelea matengenezo ya kipande cha barabara cha kilomita 33.3 cha Senkenke – Shelui kilichojengwa chini ya kiwango na kampuni China Henan International Cooperation Group Co.LTD (CHICO) kutoka China na kusimamiwa na mhandisi mshauri M/s BCEOM kutoka ufaransa.
“hii linakuwa ni fundisho kwa makapuni mengine wanaolipua lipua kazi ila napenda kuwashukuru CHICO kwa kuwa wastaraabu kukubali yaishe na  kurudi kwenye site na kurudia kujenga barabara kwa gharama zao” alisema waziri huyo wa ujenzi.
Wawakilishi CHICO kutoka China wakisikiliza maelekezo kutoka kwa Waziri wa Ujenzi Dr. John Magufuli

Aidha ametoa wito kwa Maneja wa mikoa wa wakala wa barabara nchini kuwa waangalifu kusimamia kazi hizo,kazi zingine zikiharibika meneja  wa mkoa aondoke pamoja na mkandarasi kurudia kazi.
"Tunachota na kumimina juu ya kokoto, hii ndiyo Lami bwana" Hii ndiyo aina ya ukarabati ambao CHICO wanafanya katika barabara ya Sekenke Sherui ambako makumi ya watanzania na wageni hupoteza maisha kila siku kwa ajali za magari na kusababisha mamilioni ya mali kupotea. Je, Picha hii inakupa funzo gani? Tutafika? Kazi tunayo Watanzania

Kwa upande wa meneja wa wakala wa barabara mkoani Singida Mhandisi Yustak Sylvanus Kangolle akitoa taarifa  kwa waziri Magufuli ya marudio ya matengenezo ya barabara ya kutoka mchepuo wa Sekenke hadi Shelui yenye urefu wa kilomita 33.3
Amezitaja changamoto zinazomkabili barabara hiyo ikiwa ni pamoja na kwa mkandarasi bado hajafanikiwa kupata udongo kwa ajili ya kujengea msingi wa barabara hali itakayosababisha kuchelewesha utekelezaji wa matengenezo yaliyopangwa kufanyika

Barabara ya Singida – Shelui sehemu ya mchepuo wa Sekenke hadi shelui ulikamilika mwezi wa Janauri 2008 na kipindi cha mwaka mmoja cha uangalizi wa ubora wa barabara kukamilika mwezi Januari 2009 kwa gharama za shilling billion 35 ambazo serikali ya Tanzania ilikopa kutoka banki ya dunia.

No comments: