NA Phesthow Sanga
Iramba
Viongozi 17 Wakiongozwa na Diwani Wa Kata ya Ntwike Mhe, Albart Makwala , Mwenyekiti wa Serikali ya Kijiji cha Nkonkilangi, Tano Mussau , Ofisa Tarafa, Luther Mpndu Pamoja na Wajumbe Wa Halmashauri ya kijiji hicho na Wazee Maarufu wa kijiji, katika Tarafa ya Shelui Wilayani Iramba Waliandamana kwa Mkuu wa Wilaya kutaka kujua Hatma ya Mgodi Wao.
Hatua hiyo Imejiri Baada ya siku mbili tu ya kupigwa Stop kwa mgodi huo kufanya kazi na Mahakama septemba 27 mpaka Maamuzi ya kesi mama Itakapotoa Uamuzi wa mmiliki Halali wa machimbo hayo .
Viongozi hao waliofika kwa Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yahya Ismail Nawanda na kumweleza kuwa Baada ya Mahakama kutoa Amri ya kusimamishwa kwa Shughuli Za Mgodi Mbele ya Kiongozi Wao wa Mgodi, na Anayesimamia Kesi yao dhidi ya John Bina, pamoja na kuitii Amri hiyo Lakini John Bina Amekiuka Amri halali ya Mahakama kwa Kuvamia Mgodi na kufanya Uharibifu wa Mali.
Diwani Albert Mkwala Pamoja na Viongozi Wengine Walimpa DC huyo Malalamiko kuwa John Bina na Wenzake wametia Chumvi Kwenye Mashine Nne za Kuvuta Maji Zenye Ukubwa wa Vlt 24 aina ya AMEC, kutoka China Zenye Thamamani ya Shilingi milioni Nane na Laki Nane {8.800.000.}
Aidha Wameeleza kuwa Ndani Ya Mgodi wao Kuna Jumla ya Duara Ishirini Na Moja lakini kutokana na kuwekwa Chumvi kwenye Mashine Za kupampu Maji Tayari Duara Tatu Zimetumbukia nyeye dhamani ya Milioni Mia Tatu ambazo Zilishaanza kutoa Madini Na kuanza kulipa gharama za Uchimbaji kwa Wenye Maduara hayo .
Viongozi hao wamesema kuwa Mpaka Sasa Kuna Waathirika Elfu Moja wa kiuchumi ambao hutegemea Machimbo hayo baada ya kusimama kuchimba Madini na kujipatia kipato ,”Wamesema kuwa , Licha ya hilo kuna Wananchi Elfu Tano Ambao Wameathirika Kiuchumi pia kupitia kusimamishwa kwa Machimbo hayo.” Wamekazia .
Diwani Albert Amesema kuwa Walipofika kwa DC Nawanda, hakuwa Tayari kuwasikiliza kinyume chake Alinza kuwatukana na kuwa kemea huku Akitishia kumweka ndani Emmanuel Magai na Kumwita Magai kuwa ni Mjinga kwanini hataki kuweka Mkataba na John Bina.
Hata hivyo watu hao wamedai kuwa Wao Walitii Mamlaka ya Mahakama tu kwani leseni Ya Bina Inasoma ni ya kijiji Cha Mgongo na Siyo Nkonkilangi Ambayo ndiko Ugomvi Upo na Kudai huo ni Uone vu Fulani, na Kuiomba Serikali Kuingilia kati Kusuluhisha Mgogoro huo mapema .
Juhudi za kumtafuta John Bina na Wenzake Kwa Njia Simu, Kuzungumzia Tuhuma Zinazo Mkabili Za kuweka Chumvi kwenye Mashine Za kupampu Maji kwenye Mashimo ya Maduara zimegonga Mwamba kwa kukataa Kupokea Simu ilipokuwa inaita mpaka inakatika bila majibu.
No comments:
Post a Comment