Friday, October 12, 2012

USALAMA MDOGO VITUO VYA DALADALA MWANZA

Mmoja wa Abiria kutoka Ilemela kwenda Butimba Jijini Mwanza akijaribu kuingia ndani ya daladala kupitia dirishani akiepuka vibaka katika moja ya vituo vya abiria ambavyo havina taa, jambo ambalo ni hatari kwa usalama wake na gari pia. Picha zote na Edson Raymond

Edson Raymond
Mwanza
Baadhi ya abiria jijini Mwanza wanaotumia vituo vya daladala, wameiomba serikali ya mkoani humo kuweka taa katika vituo vya daladala ili kuimarisha usalama wao pamoja na mali zao pindi wanaposubili daladala vituoni hapo.
Wakizungumza kwa nyakati tofauti na crew ya blog hii jiji humo, wananchi hao wamedai kuwa kukosekana kwa taa hizo kunasababisha kuwepo kwa giza jambo ambalo ni tahari kwa usalama pindi wawapo vituoni hapo kwa ajili ya kusubiri vyombo vya usafiri,
Imeelezwa kuwa kumekuwepo na vibaka wengi wanaojinufaisha na uwepo wa giza hilo kwa kukwapua na kupora mali zao jambo linaloonekana kuota mizizi siku hadi siku.
Abiria wakiwa gizani katika kituo cha Daladala jijini Mwanza

Wameongeza kuwa mbali na kuwepo kwa vibaka hao, pia daladala nyingi zimekuwa zikikwepa kuingia ndani ya vituo kwani abiria wengi wanasimama nje ya vituo wakikwepa giza lililopo vituoni hapo na kwenda pembezoni mwa barabara ambapo kuna mwanga wa taa za barabarani panapoonekana kuwa na usalama.
Akitoa ushuhuda wa tatizo hilo, abiria aliyejiatambulisha kwa jina la Dioniz Bundala amesema kuwa, wiki mbili zilizopita eneo la Chakechake kilipo kituo cha daladala kuna mtu mida ya usiku aliingia ndani ya gari wakati likipakia abiria na kuanza kumzonga dada mmoja akidai kwa nini amekunywa bia zake kisha akamkimbia na ghafla akamvuta dada huyo kutoka ndani ya daladala na kumwangusha chini na kumpora mkoba wake na kutoweka nao kusikojulikana.

No comments: