Bi Cecilia Munishi akitoa ufafanuzi juu ya mtindo mpya wa ukeketaji wa kutumia Tumbaku pamoja na Magadi, wanahabari wametakiwa kufanya tafiti badala ya kuamini kuwa hakuna ukeketaji unaofanyika tena mkoani Singida.
Na, Doris Meghji
Singida
Kubadilika kwa tabia miongoni mwa jamii juu ya suala la ukatili wa kijinsia hasa kwa wanawake na watoto wa kike kutategemea sana jitihata za waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuandika habari za kiuchnguzi kwa kuandika matukio ya ukatili wa kijinsia na madhara yake kwa jamii kimwili,kiakili na kisaikolojia mkoani Singida
Msisitizo huo umetolewa jana kwa waandishi wa habari wa mkoa wa Singida kwenye mafunzo yaliyoandaliwa na kituo cha Mila na Desturi Singida (SIAC) Bwana Hudson Kazonta kutokana na mila hiyo kuendelea kufanyika kwa baadhi ya watoto wa kike mkoani hapa
Bwana Kazonta anasema “kubadilika kwa jamii kutategemea sana jitihada zenu ninyi waandishi wa mkoa wa Singida kuandika habari ,makala na habari za kiuchunguzi juu ya matukio na madhara ya ukatili wa kijinsia kwa wanawake na watoto wa kike yanayotokea katika jamii ya mkoa wa Singida” alisisitiza Mwezeshaji Kazonta
Aidha amewataka waandishi wa habari wa mkoa wa Singida kutumia fursa ya mfuko wa waandishi wa habari Tanzania (Tanzania Media Fund (TMF) kupata fedha zitakazo wawezesha kuandika habari za uchunguzi lengo ni kutokomeza kabisa ukatili wa kijinsia mkoani Singida
Kwa upande wake katibu wa kituo cha mila na desturi Bi Cecila Munishi amewaomba sana waandishi wa habari kutumia kalamu zao kuelimisha jamii kutokomeza kabisa mila na desturi zilizopitwa na wakati hasa ya ukeketaji wa wanawake na mtoto wa kike mkoani hapo
“kweli elimu juu ya madhara ya ukeketaji tumetoa lakini jamii sasa imebadilisha utaratibu wa kuketa mtoto wa kike sasa wanatumia magadi na tumbaku kwa kusaga kisimi kwa madai ya kutibu ugonjwa wa lawa lawa” alisema Katibu Munishi
Hata hivyo mkoa wa singida ni moja kati ya mikoa nchini Tanzania inayofanya ukeketaji kwa baadhi ya baadhi ya makabila ya mkoa huo ikiwa ni pamoja na kabila la kinyaturu.
No comments:
Post a Comment