Na. Abdul BANDOLA
Kiongozi wa mbio za mwange wa uhuru wa Tanzania mwaka huu Kapteni Honest Mwanossa, ameeleza kuwa baadhi ya Viongozi waliopewa dhamana ya kujenga na kusimamia miradi ya maendeleo ya jamii, wameshindwa kuwa wazalendo na kwamba wanatumia madaraka yao vibaya kwa kushindwa kusimamia vema miradi ya maendeleo na rasirimali za taifa.
Kapteni Mwanossa amesema hayo katika maeneo mbalimbali nchini wakati wa mbio za mwenge wa uhuru, baada ya kukagua na kuzindua miradi ya umma na ya mtu binafsi iliyoko Singida na kubaini kuwa miradi ya watu binafsi ina ubora na viwango kuliko miradi ya serikali.
Mwanossa anasema kuwa watu wanaopewa dhamana ya kujenge miradi ya serikali, hawajengi katika viwango kama wanavyojenga miradi yao binafsi, na sikuingiza ubinafsi katika miradi ya serikali, kwani baada kukaguwa majengo mengi ya serikali yalikuwa yako chini ya kiwango na alipowauliza wasimamizi nakukili kuwa yako chini ya kiwango.
No comments:
Post a Comment