HALIMA JAMAL
Singda
HALMASHAURI ya manispaa ya Singida,imetumia zaidi ya shilingi 753 milioni kugharamia mradi wa umwangiliaji kwa njia ya matone katika kijiji cha Kisasida.
Akizungumza na mwandishi habati hii jana,mkurugenzi wa manispaa hiyo,Mathias Mwangu, alisema fedha za ujenzi wa mradi huo zimetolewa na serikali kuu kupitia mfuko wa maendeleo ya umwangiliaji wilaya (DIDF).
Alisema mfuko huo umetoa shilingi 750,000,000 na wananchi kwa upande wao, wamechangia shilingi milioni tatu.
Mwangu alisema mradi huo wa aiana yake katika manispaa ya Singida,ulianza kutekelezwa mwaka juzi na unatarajiwa kukamilika mwishoni mwa mwezi huu.
Alisema lengo la mradi,ni kuongeza uzalishaji wa mazao ya bustani kwa kutumia maji kidogo,nguvu kazi kidogo na kupunguza muda wa kumwangilia.
Aidha,mkurugenzi huyo alitaja faida zingine za mradi huo kuwa ni pamoja na uhakika wa upatikanaji wa maji kwa ajili ya umwangiliaji,kupunguza upotevu wa maji na wakulima wa vijiji vya jirani watapata fursa ya kujifunza teknolojia hiyo mpya.
“Matarajio yetu ni kwamba kupitia mradi huu,uzalishaji wa mazao ya bustani utaongezeka kutoka tani 25 hadi tani 70 za nyanya na kwa upande wa zao la kitunguu,pia utatoka kutoka tani 16 hadi 32 ifikapo mwaka 2015.Kwa hali hiyo, kipato cha wakulima kitaongezeka na kuwawezesha kuishi maisha bora”,alifafanua.
Mwangu alisema manispaa inatarajia kuongeza eneo la skimu kutoka hekta 16 za sasa,hadi hekta 32 ifikapo mwaka 2015.
“Tunachowaomba wananchi wa kijiji cha Kisasida,ni kuutunza vizuri mradi huu ili uweze kudumu kwa muda mrefu zaidi”,alisema.
No comments:
Post a Comment