Na. Boniface Mpagape na Eufrasia Mathias
Standard Radio iliyopo mjini Singida, inayoanza matangazo yake rasmi hivi karibuni itasikika pia katika mikoa mingine nchini Tanzania.
Mkurugenzi mtendaji wa Standard Radio Bw. James Daud amesema hayo wakati wa kikao na wafanyakazi wa redio hiyo ambacho kimefanyika katika ofisi za Standard Radio.
Amesema kutokana na dunia ya sasa kuwa na teknolojia ya mfumo wa digitali, Standard Radio imeanza na mfumo huo ili iweze kusikika kwa Watanzania walio wengi na kukidhi mahitaji yao ya kupata habari, kuelimishwa kupitia vipindi mbalimbali, lakini pia kuburudishwa katika usikivu wa uhakika na ulio katika viwango vinavyokidhi.
Mkurugenzi huyo amesema katika kuhakikisha lengo hilo linafikiwa mipango inafanyika ya kuweka vituo vya kukuza matangazo yaani Booster stations katika baadhi ya mikoa, lakini pia kuunganisha matangazo ya Standard Radio katika Satelaiti ambapo pia yataweza kusikika katika nchi nyingi duniani katika kipindi cha miaka mitatu ijayo.
Bw. James amesema sambamba na mikakati hiyo, Standard Radio ambayo hivi karibuni itaanza matangazo yake rasmi, pia amekwisha sajili Standard Televisheni ambayo itaanza mwaka 2015 kama mipango itakwenda kama inavyotarajiwa.
Naye meneja wa Standard Radio Bw. Prosper Kwigize, amesema wakazi wa Singida kweli walikuwa na hamu ya muda mrefu ya kuwa na kituo chao cha redio ambacho sasa tayari wanacho. Amesema jamii ya Singida imepokea ujio wa Standard Radio kwa mikono miwili kwani hakukuwa na kituo chochote cha redio isipokuwa vituo vya kukuza matangazo ya redio nyingine zinazotangaza kutoka mikoa mingine.
Bw. Kwigize amesema , Standard Radio ni ya jamii na hivyo vipindi vyake vitalenga zaidi watu wa hali duni kabisa walioko vijijini ili kuibua matatizo na changamoto zinazowakabili katika maisha yao ya kila siku ili matatizo yao yaweze kutafutiwa ufumbuzi na serikali pamoja na mashirika yanayofanya shughuli hiyo kwa lengo la kuikwamua jamii kuondokana na umaskini na kujiletea maendeleo endelevu. “Standard Radio, Sauti ya Wasiosikika”
AHADI ZA WAFANYAKAZI WA SF FM
Kazi kwa ushirikiano
Wafanyakazi wa Standard Radio FM wametoa ari ya kuwa na ushirkiano katika kazi zao kwani wanaamini kuwa ushirikiano ndo msingi wa kufanikisha malengo yao waliyojiwekea.ushirikiano huambatana na na umakini kazini hasa kufanya jambo kwa wakati na ufanisi
Wafanyakazi wa Standard Radio FM wametoa ari hiyo mbele ya mkurugenzi wao Bwana Daud James wakati wa kikao chao kilichofanyika katika studio zao zilizopo mtaa wa Ginney wilaya Singida mjini
Hata hivyo wameupongeza uongozi wa kampuni yao ya Standard Voice Limited kwa kuwapa nafasi ya kutoa maoni kuhusu mipango ya kuiendeleza kampuni yao inayotarajia kuwa kampuni ya kwanza Tanzania katika suala zima la habari na mawasiliano kwa ujumla
Kwa upande wake Mkuu wa Standard Radio FM Bwana Prosper Kwigize amewaahidi wafanyakazi kuwa atafanya kazi nao bega kwa bega ili kufikia malengo yale waliyoyapang
Hata hivyo Bw. Kwigize ameonya kuwa mfanyakazi ambaye atashindwa kwenda sambamba na dira na malengo ya kampuni hatavumiliwa zaidi ya kufukuzwa kazi na kutoa nafasi kwa wanataaluma wengine watakaokuwa tayari kufanya kazi kwa malengo
Aidha ameahidi kutoa bakshishi kwa kila mtumishi atakayeonesha jitihada zake katika kazi na kuchangia uzalishaji bora wa kazi za Radio.
Wafanyakazi wote kwa pamoja wameahidi kuhakikisha wanakwenda sambamba na dira na mtazamo wa Radio yao ili nao wafaidi ahadi zilizotolewa na viongozi wao.
Kila mmoja ameahidi kujituma na kuleta ushindani kwa mwenzake
No comments:
Post a Comment