Edilitruda Chami na
Eufrasia Mathias
Popote nakaa , popote nakula japo akili sina lakini
siathiriki
Hivi tulishawahi kujiuliza kwanini sisi watu wenye akili
timamu tukila vitu vichafu tunaathirika? Kwani vichaa hula vitu vichafu sana
lakini haitokei siku wakaumwa tumbo wala kupata maradhi kama yale tunayoyapata
sisi ikiwa ni pamoja na kipindupindu
Je, umewahi kujiuliza kwanini? Tuyaache hayo . Mimi
ninachotaka kuzungumza ni hili, umewahi kumsaidia mtu mwenye matatizo ya akili
hata siku moja? Kama ndiyo ulimfanyia nini? Kama siyo kwanini? Watu hawa ni
watu kama sisi, nao wanahitaji huduma kama sisi, wanahitaji kula, kuvaa na
kulala pia
Ona picha hii, huyu ni mtu mwenye matatizo ya akili ambaye
yuko barabarani katikati ya manispaa ya Singida, jiulize hana ndugu, hana
marafiki, au sisi hatumwoni? Au thamani yake imeisha akiwa bado duniani?
No comments:
Post a Comment