MWIGULU AKIMKARIBISHA MSIMAMIMIZI WA UCHAGUZI KUSOMA MATOKEO YA UCHAGUZI
Picha zote katika habari hii zimepigwa na Seif Takaza
NA Phesthow Sanga
Iramba
Amini Usiamini aliyekuwa Mwenyekiti wa Wilaya ya Iramba kwa miaka mitano Mkoani Singida Wilson Nico Msengi Ameshindwa Vibaya katika Uchaguzi Mkuu wa Wilaya Uliofanyika Jana September 30 katika Ukumbi wa Halmashauri ya wilaya ya Iramba.
Akisoma Matokeo hayo Baada ya Uchaguzi huo kumalizika Mkuu wa Wilaya ya Mkalama Edward Ole Lega, Alisema kuwa,Nafasi ya Mwenyekiti iliyegombaniwa na Watu watatu, Wilison Nico Msengi Aliyekuwa anatetea kiti chake Alipata kura 31 Kati ya kura 889 zilizopigwa, Moses Nalogwa Kitonka Alipata kura 364 na Charles Mkumbo Maakala Alipata kura 483 na kutangazwa kuwa mshindi na Mwenyekiti Mpya CCM Iramba .
Msimamizi Mkuu Ole Lenga aliwatangaza Wajumbe wa Mkutano Mkuu Taifa ambao iliyogombaniwa na Wagombea 14 na Waliotakiwa ni Wajumbe Watano Walioshinda ni pamoja na Mkuu wa Wilaya ya Iramba Yahya Ismail Nawanda Aliyeshinda kwa kishindo kwa kupata kura 787.
Wengine ni pamoja na Kinota Omary khamis JB, Kura 525,Amani Andrew Paulo Rai kura 524,mwingine ni Daud Amosi Madelu aliyepata kura 368 na mwanamke pekee aliyefanikiwa kupenya katika Wagombea 14 Wakiwepo wanawake wawili tu Alipata kura 350 nakutangazwa kuwa Washindi wa Mkutano Mkuu CCM Taifa.
Baada ya Matokeo hayo kutangazwa Aliyekuwa Mtetea kiti, Wilison Msengi Alilala na hakuwa na Uwezo Wakusema lolote juu ya kushindwa kwake Vibaya hivyo,
MWENYEKITI MPYA WA CCM CHARLES MAKALA
Mwenyekiti wa Muda wa Uchaguzi huo Mbunge wa Jimbo la Iramba Magharibi Mwigulu Nchemba aliwashukuru wajumbe kwa kujitokeza kwa Wingi na kufanya Uchaguzi bila Vurugu na kwa Utulivu Mkubwa ,mwigulu Alitoa shilingi m.2 kama Chakula kwa Wajumbe waliotoka katika kata 17 katika Jimbo lake kwa ajili ya Uchaguzi huo .
No comments:
Post a Comment