Wednesday, October 31, 2012

MAWAZIRI NAO WAJITOSA- SANAA ZATUMIKA UCHAGUZI MKUU WA WAZAZI CCM

Mmmoja wa wapambe wa mgombea wa nafasi ya ujumbe wa halmashauri kuu ya CCM kuitia umoja wa wazazi Tanzania Bw. Kirigini Paul. Sanaa na utamaduni nao ukitumiwa vizuri kama hivi katika siasa nina hakika kuwa kuporomoka kwa maadili kunaweza kumalizika. hebu fikiria kijana huyu kaamua kutumia sanaa ya asili (muziki na zana za asili) kumndadi Kirigini je atathaminiwa na wanasiasa au anatumika tu kwa kampeni.

 
Ukumbi wa Nyerere katika chuo cha Mipango ndipo uchaguzi unakofanyika,
 
Paul Kirigini mgombea aliyekuwa akipigiwa debe na makumi ya vijana kutoka mkoa wa Mara waliokuwa wakimnadi pia mgombea wa nafasi ya mwenyekiti Abdalla Bulembo, hadi naingia mtamboni zipo fununu kuwa wote hawa wameshinda
 
Adam Malima (kulia) Mgombea wa nafasi ya NEC kutoka WAZAZI akiwa katika harakati za kampeni ndani ya ukumbi, kushoto ni Mkuu wa wilaya ya Karatu Mh. Daud Felix Ntibenda (KIJIKO) Adam Malima fununu zinataja kuwa nae ameshinda, hata hivyo matokeo bado
Mh. Vita Kawawa  mgombea nafasi ya NEC akiwa katika harakati za kushawishi wajumbe wampe kura za ndiyo awe mjumbe wa halmashauri kuu ya CCM taifa, ushindani wa nafasi hii ni mkubwa kwani wagombea wote ni vizito na wenye majina makubwa. yetu macho je watakivusha chama 2015?
 
 
 

ALIYEJENGA JIRANI NA MAWE HAYA ALIFIKIRIA KIASI CHA KUTOSHA? SERIKALI IPO HAPO?



Na Edilitruda Chami

Ewe binadamu umewahi kujiuliza ni kwa kiasi gani unathamini uhai wako? Kama unahisi unauthamini je ni vigezo gani vinavyoashiria kwamba unauthamini? Kwa nini tusithamini uhai tulio nao na kufanya maisha kuwa  mafupi?

Singida ni mkoa wenye miamba mingi na miamba hii imekuwa ikivutia watu wengi huku watalii wakifika katika mkoa huo kutalii ila watu wa mkoa  huo wamekuwa wakitumia miamba hiyo katika mazingira hatarishi huku wengine wakidiriki kujenga karibu na miamba hiyo ambapo ni hatari kwa maisha yao
 

JE BINADAMU HUYU KWA WATANZANIA HANA THAMANI?



Edilitruda Chami na Eufrasia Mathias

Popote nakaa , popote nakula japo akili sina lakini siathiriki

Hivi tulishawahi kujiuliza kwanini sisi watu wenye akili timamu tukila vitu vichafu tunaathirika? Kwani vichaa hula vitu vichafu sana lakini haitokei siku wakaumwa tumbo wala kupata maradhi kama yale tunayoyapata sisi ikiwa ni pamoja na  kipindupindu

Je, umewahi kujiuliza kwanini? Tuyaache hayo . Mimi ninachotaka kuzungumza ni hili, umewahi kumsaidia mtu mwenye matatizo ya akili hata siku moja? Kama ndiyo ulimfanyia nini? Kama siyo kwanini? Watu hawa ni watu kama sisi, nao wanahitaji huduma kama sisi, wanahitaji kula, kuvaa na kulala pia

Ona picha hii, huyu ni mtu mwenye matatizo ya akili ambaye yuko barabarani katikati ya manispaa ya Singida, jiulize hana ndugu, hana marafiki, au sisi hatumwoni? Au thamani yake imeisha akiwa bado duniani?

WEST PRODUCT VS HUMAN HEALTH IN TANZANIA


 
By Eufrasia Mathias

It is at least six years since Tanzania held the campaign against use of plastic bags demanding that the  use of plastic bags destruct the environment due to their hardness hence they prevent the penetration of water in the soil and cause soil destruction

During the campaign the environmental look changed because there was no scattered plastic bags around the environment and every person tried to be part of the campaign by burning any misplaced plastic bag

It seems that it is not culture and behavior of some Tanzanians to be clean; they do cleanliness only when they are told to do so by either the government, private or public association. Cleanliness is health in the sense that the clean area has no outbreak of diseases

The campaign against the use of plastic bags died just after the government was quiet about it, because it is not the culture of Tanzanians to do cleanliness the plastic bags are turned to be flowers of decorating the streets

Responsible people, please remind people to do cleanliness?

 

 

 

 

MAJI BADO NI MSIBA SINGIDA


 
Ama kweli maji ni uhai

Na Eufrasia Mathias

Ikiwa imebaki muda usiopungua miezi miwili kukamilka kwa mradi wa maji mkoani Singida bado hali ya maji inazidi kuwa tete kiasi kwamba watu wanatamani kuhamia maeneo ambapo kuna visima na mabomba yanayowategemeza watu wa maeneo husika ili tu waweze  kuwahi foleni ambayo hutokea na kufurika maeneo hayo wakati  maji yanapoanza kutoka

Kwa ujibu wa Meneja wa Mamlaka ya maji manispaa ya Singida SUWASA Mhandisi Kombe Mushi,  mkandarasi wa mradi wa maji  unaojengwa anatarajiwa kukabidhi mradi huo Desemba 31, 2012. Kwa hali halisi ilyopo eneo la ujenzi huo sina uhakika kama miezi miwili itatosha kukamilisha ujenzi huo

Ukitazama mabomba yaliyoko nje ya eneo la ujenzi ambayo yanatakiwa yatumike kukamilisha mradi huo unaweza kukadiria muda mrefu zaidi unahitajika kukamilisha mradi huo. Swali ni kwamba mradi unajengwa, wakazi wa Singida watateseka mpaka lini?

Inashangaza kuona mtoto mdogo kazidiwa na kiu hadi anataka kutumbukia katika dumu tupu lililopo kwenye foeni inaosubiri maji yatoke baada ya muda usiojulikana. Jamani tuwe na mawazo mapana

 

Thursday, October 25, 2012

Kerosene! Diesel! Petrol! Where are you?


By Eufrasia Mathias

Singida is the central region in Tanzania where many of the cars and buses pass by on the way to their long journeys. Possibly every person having the vehicle, bus or any other car passing in Singida expect to have break at Singida where he or she can have lunch so as to release the tension of the journey and gain new power for continuing with the journey

Not only getting lunch but also people plan to feed their cars and buses at Singida, but you can be surprised to see how the fuel stations are crowded and even people fight for oil to feed their vehicles instead of ordering the petrol while resting with the bottles of drink on their hands

It is almost two weeks since there is scarcity of Kerosene and Diesel in Singida, many cars and vehicles are even parked because of this problem and some of the fuel stations are closed

Question: is it that there is no kerosene and Diesel in Tanzania especially in Singida?

The answer is no, there is much kerosene and diesel in Tanzania, particularly in Singida “BUT THE PROBLEM IS REDUCTION OF THE PRICE”

Solution: the responsible people in price moderation should take measure on it to save the life of Many Tanzanians otherwise “If we are not careful there is possibility of becoming THE POOREST COUNTRY”

WOMEN CAN BE USED TO CHANGE THE WORLD


By. Eufrasia Mathias, Standard Voice Journalist
 
Women are the most people who engage in Entrepreneurship. Most women who are entrepreneurs are the one who are independent and their families depend on them in provision of basic needs like clothes, shelter and food

Singida is one among the areas with women who are entrepreneurs and they do their best to take care of their families using the money from their businesses. The most businesses they engage in are like beauty salon, cafeterias and small areas of selling fruit broadly known as “vibanda vya matunda”

“Mama Prosper” known as Mary Luya is the successful woman in Singida who own the cafeteria and this business gives her enough money to provide the needs in her family. As hard working woman and the boss in the business she took initiative of preparing the food for her customers as good as possible and she always train other workers in her business to patient to the customers because customers need care all the time 

Tuesday, October 23, 2012

OUR AUDIENCE IN THE LAST 7 DAYS

 
 Here is our audience detail found in our on line audience survay, check out and join us
 
 
 
United States
 
 
 
 

 
 
386
Tanzania

244
 
United Kingdom
 
 39
Russia

34
Kenya

31
France

12
Belgium

3
Malaysia

3
Japan

1
South Africa

1

MKE AUWAWA KWA WIVU WA MAPENZI

Kamanda wa Jeshi la Polisi mkoa wa Singida ACP Linus SInzumwa akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake
 NA. HALIMA JAMAL
Singida  MCHIMBAJI mdogo wa madini mkazi wa kijiji cha London wilaya ya Manyoni mkoa wa Singida,Joshua Lazaro (46),anashikiliwa na jeshi la polisi kwa tuhuma ya kumuuwa mke wake Tatu Mathias(46) kwa madai kuwa anatembea nje ya ndoa. Akizungumza na waandishi wa habari juzi jioni ofisini kwake, kamanda wa jeshi la polisi mkoa wa Singida,Linus Sinzumwa,alisema tukio hilo la kusikitisha,limetokea oktoba 21 mwaka huu majira ya jioni. Alisema mauaji yaho yamechangiwa na wivu wa mapenzi uliopitiliza ambapo Joshua alikuwa anamhisi mke wake Tatu,anatembea nje ya ndoa. Sinzumwa alisema mtuhumiwa Joshua alimchoma mke wake tumboni na chuma na kusababsiha utumbo wote kumwagika nje na kusababisha kifo cha Tatu papo hapo.Mtuhumiwa Joshua alikamatwa muda mfupi baada ya kufanya mauaji hayo. Kamanda huyo alisema upelelezi utakapokamilika,mtuhumiwa Joshua atafikishwa mahakamani kujibu tuhuma inayomkabili. Katika tukio jingine,Sinzumwa alisema lori aina ya Volvo T.210 CDZ lililokuwa linavuta tela T.964 CBV,limeteketea kwa moto na tela lake, baada ya kutokea kwa hitilafu ya umeme. Alisema tukio hilo limetokea oktoba 21 mwaka huu, saa tisa alasiri katika barabara kuu ya Singida- Mwanza katika eneo la kijiji cha Nkwae wilaya ya Singida. “Pamoja na lori hilo na tela lake kuteketea kwa moto,pia mitumba mbalimbali na shehena ya viatu vilivyokuwa vinasafirishwa kutoka Dar-es-salaam kupelekwa jijini Mwanza,navyo vimeteketea.Ni mitumba na viatu vichache vimeokolewa.Hadi sasa bado hatujafahamu thamani ya uharibifu huo mkumbwa”alisema. Kamanda Sinzumwa alisema lori hilo siku ya tukio,lilikuwa likiendeshwa na Daud Kanoni Mwakatobe (36) mkazi wa jijini Mbeya.Uchunguzi zaidi kuhusiana na moto huo,bado unaendelea.

WANAHABARI SINGIDA WANOLEWA

Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makni kumsikiliza mwezeshaji katika mafunzo ya sera na ufuatilaji wa bajeti ukumbi wa social training centre manispaa ya singida
 
NA, Doris Meghji

Singida

Elimu ndogo ya uchambuzi wa sera miongoni wa waandishi wa habari nchini ni sababu kuu mojawapo inanyopelekea kutohabarisha umma juu ya mambo mbali mbali ya maendeleo imefahamika.

Hayo yamebainika leo mkoani Singida kwa waandishi wa habari mkoa wa singida katika mafunzo uchambuzi wa sera na ufuatiliaji wa bajeti(policy analysis and budget tracking) yaliyoandaliwa na Muungano wa vilabu vya waandishi wa habari Tanzania(UTPC) kwa waandishi wa habari wa mkoa huu.

Akiongea na Standard Radio Mwezeshaji wa mafunzo hayo Bwana Adam Ndokeji toka mwanza amewataka waandishi wa habari kubadilika kwa kufanya uchambuzi wa sera mbali mbali za masuala ya maendeleo lengo likiwa ni kuuhabarisha umma kwa mambo ya kimaendeleo.


Naye mmoja wa waandishi wa habari wa mkoa wa singida Bi Awila Silla anasema “nimefurahia sana mafunzo hayo ingawa yamechelewa kujifunza kwani tayari tulishavirunda kuripoti mambo mengi ya maendeleo katika umakini na umahususi unaotakiwa,hata hivyo ni wakati muufaka sasa wa mtazamo chanya kuahidi kuwa elimu ya mafunzo haya itaondoa mapungufu yote ya nyuma”amesisitiza Bi silla.

Katika mafunzo hayo jumla ya waandishi kumi na nane(18) wanapatiwa mafunzo hayo mkoani singida yatakayodumu kwa kipindi cha siku nne.

POLISI WASHIRIKI MAHAFALI SHULE YA MSINGI

Baadhi ya wanafunzi wakifuahia jambo wakiwa pamoja na mtoto wa rais Kikwete Ndg. Ridhiwani. Picha na mtandao wa google.
 
Na Daud Nkuki
Singida Oct 23, 2012
Wazazi na walezi wamekumbushwa kuzingatia wajibu na majukumu yao ya kuwalea na kuwaendeleza watoto wa kielimu.
Mkuu wa kituo cha Polisi Mtinko, wilaya ya Singida vijijini, Inspekta Iledefonce Bernard Kagaruki, ambaye alikuwa mgeni rasmi, aliyasema hayo katika sherehe za mahafali ya 35 katika shule ya msingi Malolo wilayani humo.
Inspecta Kagaruki amewaangaliza kuhusu umri mdogo wa kumaliza elimu ya msingi ambao ni kati ya miaka 12 na 14, hautawasaidia wazazi katika shughuli za kimaendeleo ambazo huhitaji zaidi nguvu kazi, wanaporudi kijijini.
Ameendelea kuwaasa wasiridhike na kiwango cha elimu hii bali iwe ni kichocheo cha kuendelea na elimu ya juu ya sekondari wala wasiwe na tamaa ya kuwaoza au kuswaga ng’ombe huko porini.
“Watoto watakaofanyiwa vitendo hivyo, waripoti polisi ili sheria ichukue mkondo wake” aliagiza.
Kusoma sio lazima kuajiriwa, kwa elimu hiyo kile watakachokifanya hakina budi kibadilishe maisha yao na ya wazazi wao.
Uwezo wa kushiriki vyema na kuzingatia elimu wanayopewa watoto ni pamoja na kupatiwa chakula cha mchana ambacho hakina budi kuwekewa mkazo na wazazi ama walezi.
Aidha wale wenye dhamana ya kutunza mifuko ya chakula cha wanafunzi, wawe waaminifu kulingana na mahitaji ya watoto.
Jumla ya wanafunzi 112 kati ya 176 wakiwemo wasichana 63 na wavulana 49 wamehitimu elimu ya msingi shuleni hapo .
Mwisho

Sunday, October 21, 2012

MINADA MKOANI SINGIDA NA HATAARI KWA MAZINGIRA NA AFYA

Na Edilitruda Chami
 
Wengi tumekuwa tukijiuliza maana halisi ya neno mazingira, ila tafsiri zimekuwa ni nyingi wengine husema ni kitu chochote kinachomzunguka binadamu, wengine husema ni sawa na usafi huku wengine wakihusisha pia uoto wa asili yaani nyasi na miti, vyanzo vya maji, mito na milima.
 
Katika eneo la mnadani mkoani Singida hali inaendelea kuwa mbaya zaidi siku hadi siku kutokana na mazingira kuwa machafu huku maji ya kusafishia vyombo na  mazingira yakizidi kuadimika siku hadi siku.  
 
Ulevi ,uchafu, uhaba wa maji, huku omba omba wakiwa wametanda kila upande, yote haya yamo katika soko la mnadani njia panda ya kwenda Arusha-Makyungu mkoani Singida. Biashara ya pombe za kienyeji imechukua eneo kubwa la soko tofauti na bidhaa nyingine, omba omba nao kila jumamosi wanahamia katika soko hilo kwa lengo la kutafuta ridhiki ili kujikimu na hali ngumu ya maisha, wengi wao wakiwa ni wazee pamoja na watoto wadogo.           Bi. Edilitulda Chami, Mwandishi wa habari
 
Mazingira ya soko hilo yamekuwa kero kutokana na uchafu na harufu mbaya ya pombe za kienyeji maarufu kama Mtukuru ( lugha ya Kinyaturu ) ambazo zimekuwa zikinyweka katika hali ya uchafu wa hali ya juu. Pombe hiyo ya kienyeji imekuwa ikitumika kama maji ya kunywa kwani hata watoto wadogo hununua maandazi na pombe hiyo kwa lengo la kupunguza kiu na njaa.  Ni vyema sana kulinda tamaduni zetu kama matumizi ya vyakula, vinywaji na mengineyo, lakini usafi uzingatiwe!
 
 
Hali hii si kwamba imeonekana kwa mwandishi wa habari tu, eneo la mnadani Singida kutokana na umaarufu wake pia hutembelewa na maafisa wa ngazi mbali mbali wa serikali ambao kila jumamosi huhudhuria hapo kunywa pombe na kula nyama choma na supu. Wengine wanashiriki hata katika mlo wa mchana katika eneo hilo, najiuliza je hawaoni hali hii?
 
Waswahili walisema, usipoziba ufa basi jiandae kujenga ukuta. Endapo utatokea ugonjwa wowote wa mlipuko huenda ukagharimu maisha ya watu ambayo hayalinganishwi au kuthamanishwa na chochote hapa duniani.
 
 

WATUMA SALAAMU WATOA MISAADA KWA WATOTO VIZIWI


Na.  Boniface  Mpagape.

Chama cha watuma salaam kupitia vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini, kimetoa msaada  kwa watoto  viziwi wanaosoma katika shule ya msingi Tumaini iliyopo katika manispaa ya Singida.

Watuma salaam hao nchini  wametoa msaada wa vitu mbali mbali vikiwemo sabuni, mafuta ya kupikia, sukari, chumvi na fedha taslim shilingi laki moja.

 Katika risala yao watuma salaam hao nchini wamesema  ni vyema pia kwa taasisi nyingine na watu wenye mapenzi  mema  nchini kuiga mfano wa kutoa misaada kwa watu wenye mahitaji na kutoiachia jukumu hilo serikali pekee.  Wamesema misaada kama hiyo imetolewa pia katika mikoa mingine ikiwemo Arusha, Iringa, Mbeya, Morogoro, Manyara, na Dodoma. Aidha wametoa wito kwa jamiii kujihadhari na ugonjwa wa UKIMWI.

Mgeni rasmi katika hafla hiyo, Bi. Christina Mwamgomo  Meneja wa Benki  ya NMB tawi la Singida mjini, amewapongeza wanasalaam hao kwa moyo wa huruma na kuamua kutoa msaada kama huo na kwamba wanatakiwa wawe mfano wa kuigwa katika jamii ya Tanzania. Amewaomba waendelee  kuwa na upendo na mshikamano na kusisitiza taasisi nyingine kushiriki katika kutoa misaada kwa watu wanaoihitaji kama walemavu.

Wanasalaam hao nchini wamekutana katika kongamano lao ambalo hufanyika kila mwaka, ambapo mwaka huu limefanyika Oktoba 20 Singida mjini.  Katika hafla fupi ya kutoa msaada kwa watoto viziwi, ambayo pia ilihudhuriwa na wawakilishi kutoka vyombo mbali mbali vya habari hapa nchini, mwakilishi wa Radio Clouds FM ametoa shilingi laki moja, meneja wa NMB Singida ametoa shilingi laki moja, pamoja na wanasalaam kuchanga shilingi elfu sitini na mbili papo hapo na kufanya jumla ya fedha taslim zilizochangwa kuwa shilingi laki tatu na sitini na mbili elfu.

Shule ya msingi Tumaini viziwi ina jumla ya wanafunzi themanini na mbili, wavulana arobaini na tano na wasichana thelathini na saba. Shule hiyo ina walimu wanane na inakabiliwa na changamoto mbali mbali ikiwemo mahudhurio hafifu yanayosababishwa na  baadhi ya wanafunzi kutoka  umbali wa kilomita tisa, upungufu wa vyumba vitatu vya madarasa, nyumba za walimu na chumba cha kupima usikivu (Audiometry room).  Pia baadhi ya wanafunzi huacha shule kutokana na kuishi mbali na shule.  
Baadhi  ya mikoa iliyowakilishwa na wanasalaam ni Singida, Katavi, Simiyu, Morogoro, Manyara, Arusha, Mbeya

Thursday, October 18, 2012

RPC SINGIDA AZUNGUMZA NA VIONGOZI WA DINI

Na, Khadija Mahamba 

Singida
Kufuatia kuwepo kwa vurugu za kidini nchini Tanzania zilizopelekea kuchomwa kwa makanisa kadhaa nchini, jeshi la polisi mkoani singida linafanya mazungumzo na viongozi wa dini kwa lengo la kutafakari hali hiyo na kutafuta ufumbuzi wa hali hiyo.
Kamanda wa polisi mkoa wa singida Kamishna msaidizi wa Polisi Linus Sinzumwa leo amekutana na viongozi wa dini ya kikristo mkoani humo huku akiahidi kukutana tena na viongozi wa dini ya kiislamu ijumaa October 19, 2012
Aidha katika mipango ya jeshi hilo, kamanda Sinzumwa October 22 mwaka huu, anatarajia kuwakutanisha viongozi wa dini zote mbili wakristo na waislamu kwa lengo la kujadiliana kuhusu namna ya kumaliza tofautii zao na kukomesha vurugu za kidini nchini.
Hata hivyo kamanda Sinzumwa amekataa kueleza mazungumzo hayo yalivyokuwa kwa madai kuwa umakini unahitajika kabla ya kuyatangaza mazungumzo yao na kwamba atafanya hivyo baada ya kukutana na pande zote mbili.

WAWILI WAFA KWA AJALI SINGIDA.


Na Edilitruda Chami na Abduli Bandola
Watu wawili wamefariki dunia kwa ajali mbili tofauti mkoani Singida,  ikiwemo ya mtu mmoja kugongwa na  gari na mtu mwingine  kuanguka kwa pikipiki iliyokuwa katika mwendo kasi  na kusababisha  kifo.
Akizungumza  na Standard Radio Kamishina Msaidizi wa Jeshi la Polisi Mkoa wa Singida ACP Linus Sinzumwa  amesema kuwa mtu mmoja aliyefahamika kwa jina moja la Mussa (23),  amegongwa na kufa papo hapo na gari lenye namba za usajili T 887 BFS aina ya Scania, mali ya Benevoti Jovin likiendeshwa na Shaban Abbas  lililokuwa likitoka Dar-es-salaam kuelekea Nzega . Ajali hiyo imetokea maeneo ya kibaoni manispaa ya Singida Oktoba 16, 2012.
Amelitaja tukio la pili kuwa  ni  la dereva wa pikipiki yenye namba za usajili T 278 BAH  aina ya LUG SUN aliyefahamika kwa jina la Mustafa  Museko kufa papo hapo baada ya kuwa katika mwendo kasi  na kusababisha ajali iliyomsababishia mauti. Amesema  pikipiki iligonga mti katika kijiji cha Malima wilaya ya Ikungi  usiku wa kuamkia terehe 18 Oktoba  2012.
Kamanda Sinzumwa ametoa wito kwa wananchi kuwa makini katika utumiaji wa alama za barabarani na kupunguza mwendo kasi ili kupunguza ajali za mara kwa mara ambazo zimekuwa zikitokea siku hadi siku.

HATARI MANSPAA YA SINGIDA-MAJI HAKUNA


Wakazi wa eneo la Ginnery Kata ya Mandewa manispaa ya Singida, wakiwa wamekusanyika katika moja ya gati la maji kupata huduma hiyo.

Na  Abdul Bandola.

Mkoa wa Singida unakabiliwa na tatizo la uhaba mkubwa wa maji ambalo limefanya baadhi ya watu kuacha kufanya shughuli za maendeleo na kulazimika kutembea umbali mrefu na kutumia muda mwingi kutafuta maji.

Hali hiyo inatokana na kuchelewa kukamilika kwa mradi mkubwa wa maji unaojengwa katika kijiji cha Mwankoko katika manispaa ya Singida chini kampuni ya Spencon ya nchini India, ulitarajiwa kukamilika mwezi April mwaka 2012 lakini hadi sasa bado haujakamilika.

Akizungumza na Standard Radio ofisini kwake, Meneja wa Mamlaka ya maji manispaa ya Singida  SUWASA Mhandisi Kombe Mushi, amesema mkandarasi wa mradi huo ameahidi kukabidhi Desemba 31, 2012.

Aidha mhandisi Mushi anaunga mkono ucheleweshaji huo huku akitaja kuwa ucheleweshaji huo umetokana na kucheleweshwa kwa pampu za maji ambazo zinashikiliwa bandarini Dar es salaam na mamlaka ya mapato Tanzania TRA kwa madai kuwa hazijalipiwa kodi.

Hata hivyo uchunguzi wa standard blog umebaini kuwa madai hayo na lawama dhidi ya TRA ni matokeo ya mipango mibovu ya Halmashauri kwani miradi ya jamii zana zake kuondolewa kodi baada ya rasimu ya mradi na mapendekezo ya vifaa kuwasilishwa TRA kuombewa kuondolewa kodi.

eneo la chanzo cha maji Mwankoko kikiendelea kujengwa, wanaoonekana ni mafunzi wa TANESCO wakifunga mtambo wa umeme. picha zote na Doris Meghji

Hadi sasa mradi huo umegharimu shilingi bilion 23 na yapoo mashaka kuwa ahadi ya kukamilika mwezi desemba ni ya kufikirika kulingana na kasi ya ujenzi wake

KNOW THE WAY YOU DECIDE TO LIVE


By Boniface Mpagape.
Experience shows that many people do say “Life has no formula” and if someone succeeds, others do say its God’s Blessing, today I have learned that there is a formula of life.
 I and my fellow staff were talking to our Director, (Standard radio director) Mr. James Daud who told us there is a formula of life.  He told us that the formula of life is E + R = O.  Let me elaborate the abbreviations. E stands for an (EVENT) + R which stand for (RESPONSE) which is equal to O, an (OUTCOME).  In a simple language an Event is the ACTION plus RESPONSE; that is the way you respond to the action, in other word is PERFORMANCE which can be positive or negative depending on how you treated an event.  If the outcome is poor then you have to change your response, but if you work hard you can receive good profit in a case of business or good salary if you are an employee.  Picture: Mr. James Japhet Daud  
                                                                                                                    Managing Director
                                                                                                                    Standard Voice LTD
Mr. Daud elaborated more by giving examples; “For instance two persons receive 1 million as a salary per month that is an event; but how are they going to use the money is different.  One may spend the money extravagantly, profligately, wastefully,   while the second one may invest in establishing a barber shop etc.  Automatically the outcome can’t be the same! ”

picture: Some of Standard Radio staff in the official workshop senssion held at Singida main station

He added if someone is thinking about an event, there is always visualization in the mind which is very important.  Someone has to visualize be it in sound, mind, color etc.  Also there is subconscious mind, which is hidden plus RAS which is an abbreviation of Reticular Activating System or arrangements, whereby every human being has got it in mind, but others die without using it; they die while their minds are still new.  That is real the way you decide to live.  

M23 WITH SUPPORT FROM RWANDA AND UGANDA

picture: M23 spokesman

The recent release of a UN report claims that Uganda and Rwanda jointly financing arming and running the DRC rebels. The report which was done by UN experts. I seriously fail to see how both countries would benefit from an unstable neighbour and i have serious doubts on these western backed fact finding missions. the other day didn't they accuse Ghana of harbouring mercenaries allegedly plotting to oust the Ivorian government and even it turns out that one of the reports on genocide on hutu refugees by Rwandan soldiers was found to be deeply flawed to the point of being fictitious, and do you remember in the 90's when the WHO an agency of the UN kept giving numbers of people dying of HIV/AIDS the numbers didn't add up cause when calculated it showed that close to 70% of Africans had AIDS or had died from AIDS. The UN is controlled by the west and whatever the say goes i fear that this particular report has an ulterior motive. I'm not saying that M7 and Kagame are saints but i fail to see the benefit in helping M23 rebels

UN experts say Rwanda and Uganda backing DR Congo

(AFP)

UNITED NATIONS — A UN expert panel accused Rwanda's defense minister of being the "de facto" commander of a rebellion in eastern Democratic Republic of Congo, according to a confidential report seen by AFP.

The report accused both Rwanda and Uganda of arming and supporting the M23 rebels, whose members are former fighters in an ethnic Tutsi rebel movement theoretically integrated into the Congolese military under a 2009 peace deal.

This is not the first time the two central African nations have been accused of backing rebels in a proxy war in eastern Congo, allegations they have consistently denied.

In June, in an interim report, the same UN panel said it had "overwhelming evidence" that senior Rwandan Defense Forces officers "have been backstopping the rebels through providing weapons, military supplies, and new recruits."

In the updated, more detailed report, the experts -- who are tasked with monitoring the implementation of UN sanctions in Congo -- said they have "found no substantive element of its previous finding which it wishes to alter."

The report alleged that the M23 "de facto chain of command includes General Bosco Ntaganda and culminates with the Rwandan minister of Defense, General James Kabarebe."

The renegade general Ntaganda is wanted for war crimes by the International Criminal Court.

The report said the government of Rwanda continues to violate the arms embargo through direct military support to M23 rebels, encouraging Congolese soldiers to desert, and providing arms, intelligence and political advice.

And in Uganda, senior officials gave support "in the form of direct troop reinforcements in DRC territory, weapons deliveries, technical assistance, joint planning, political advice and facilitation of external relations."

The report said Ugandan and Rwandan military units jointly supported M23 in a series of attacks in July 2012 to take over the major towns of Rutshuru territory and a Congolese military base, Rumangabo.

During the July clashes, a UN peacekeeper from India was killed.

According to the experts, "the rebels expanded their control over Rutshuru territory with extensive foreign support in July 2012 and have recently taken advantage of an informal ceasefire to enhance alliances and command proxy operations elsewhere."

They added that "the use and recruitment of child soldiers by armed groups, notably by M23, has increased," with "the enrollment and training of hundreds of young boys and girls" and "certain M23 commanders have ordered the extra-judicial executions of dozens of recruits and prisoners of war."

Both Rwanda and Uganda have again denied strenuously that they support the M23 rebellion.

Rwandan foreign minister Louise Mushikiwabo accused the authors of the report of mounting a "determined political campaign opposed to resolving true causes of conflict" in the Congo.

Her Ugandan counterpart, Henry Okello Oryem, called the report "a joke" and called on the experts to produce their evidence.

He told AFP Ugandan President Yoweri Museveni will continue mediation efforts in the region, saying leaders there would give no credit to UN report.

The M23 rebel fighters were incorporated into the DR Congo army in 2009 as part of a peace deal in the troubled, mineral-rich eastern region. They quit the army this year in a dispute over salaries and poor conditions.

Copyright © 2012 AFP. All rights reserved
.

Wednesday, October 17, 2012

MSINDAI AIBUKA KIDEDEA CCM SINGIDA

Mgana Msindai mwenyekiti mpya wa Chama Cha Mapinduzi mkoa wa Singida

Na. Doris Meghji
Mgana Izumbe Msindai ameibuka kuwa mshindi katika uchaguzi wa uenyekiti wa Chama cha mapinduzi mkoa wa Singida  mkoa  jana uliofanyika katika ukumbi wa chuo cha Utumishi wa Umma manispaa ya Singida

Waliogombea nafasi hiyo ya mwenyekiti ni Bw. Jorum Sima Alute aliyepata kura 194, Amani Andrew Rai aliyepata kura 238 na Mgana Izumbe Msindai aliyepata kura 407 kati ya kura  837 zilizopigwa  na kuufanya uchaguzi urudiwe ambapo Mgana Msindai alipata kura 673  na Amani Rai alipata kura 41 kati ya kura halali 714 


VITUKO VYA KAZI NI UBUNIFU, UMAKINI NA MAANDALIZI

Mfanyakazi wa aina yoyote hulenga kufikia malengo bila kuwa na athari katika eneo lake, na maandalizi ndiyo njia pekee inayomwezesha mfanyakazi yeyote kufikia malengo yake.
Wakati mwingine tunalazimika kufanya kazi katika amazingira magumu lengo tu ni kuhakikisha tunafanikisha tuliyopanga kama malengo yetu ya simu
Angalia picha katika ukurasa huu juu na chini, hawa ni watu makini walioko katika malego na harakati za kuyafikia
Hapa wanajiandaa kuingia katika moja ya ofisi za umma, hivyo wanajiweka sawa kabla kwa kuweka safi nywele, hii ina maana kuwa unadhifu ni muhimu sana uingiapo katika ofisi yoyote
PICHA YA PILI

Huyo ni mwanahabari makini bila kujali kuwa hapa ni barabarani na kwamba inaweza kutokea gari au chombo chochote cha usafiri anachukua pozi na kupiga picha ya tukio muhimu, kweli uandishi wa habari hasa za picha ni wito, wengine wanalala hadi chini au kujificha vichakani ili kupata picha nzuri, si unajua tena baadhi ya wanene (boss) hawataki kupigwa picha au miradi yao kuonekana. Pig up dada
PICHA YA 3 -MASIKITIKO
Watu wengi hushindwa kutofautisha muonekano wao na mazingira waliyomo, hii imekuwa kama ni jambo la kawaida kabisa katika jamii yetu. si ajabu kwa mtanzania kuvaa nguo ya ofisini akiwa disko, wengine wanavaa mavazi ya kuogelea wakiwa vyuoni au hata ofisini, wala huoni hatari kumuona binadamu akivaa chupi na sidiria pekee awapoo barabarani au hata katika kumbi za starehe na burudani, mbaya zaidi hushangai kumuona jamaa yako akicheka na kutabasamu penye majonzi na masikitiko. Kwa wanahabari hawa wa kampuni ya STANDARD VOICE LTD hali ni tofauti, wawapo ofisini, wawapo mtaani maeneo ya raha, maeneo ya matatizo na maeneo ya kazi za uandishi wao wanafanana na mazingira hayohayo
Wafanyakazi wa standard Radio fm, wakiwa msibani katika kijiji cha Mwankoko Singida ambako mmoja wa wakazi wa kijiji hicho alitekwa na kukatwa mkono kwa imani za kishirikina na kisha kuuwawa kwa kuchomwa moto.
Picha zote na Prosper Kwigize SRfm

Tuesday, October 16, 2012

RPC LIBERATUS BARLOW AAGWA MWANZA

Jeneza alimohifadhiwa Marehemu Kamanda Barlow likiwekwa sehemu maalumu ya kuagwa, umati mkubwa wa wananachi na viongozi wa umma na vyombo vya dola walijitokeza kumuaga kabla ya kusafirishwa kwenda Dar es salaam

Mungu aliumba na kutupa pumzi ili tuishi na kuipendezesha dunia lakini Majambazi wanakatili maisha yetu, Mungu alimpenda Barlow lakini Majambazi wamemkatili


baadhi ya waombolezaji wakiwa wamezirai kufuatia uchungu wanaoupata wa kuondokewa na kipenzi chao RPC Barlow

Monday, October 15, 2012

CHF YATOA SOMO KWA MADIWANI SINGIDA

 
Na. Elisante John, Singida.
 
MADIWANI wa wametakiwa kuhamasisha wananchi kujiunga na mfuko wa afya ya jamii (CHF), ili wanufaike na huduma bora za tiba, wakati wanapougua.
Changamoto hiyo imetolewa na afisa operesheni, bima ya afya (NHIF) mkoa wa Singida, Isaya Shekifu, wakati akijitambulisha kwa madiwani wa halmashauri ya wilaya ya Singida.
Aidha Shekifu amewaomba madiwani kujiunga na mfuko huo, ili wao na familia zao waweze kunufaika na huduma zinazotolewa na CHF.
Amesema kutokana na ukweli kuwa wananchi wengi hawana uwezo mkubwa kifedha, njia nzuri na ya uhakika kupatiwa tiba sahihi wanapougua, ni kujiunga na mfuko huo.
Shekifu amesema ili kaya ijiunge na mfuko huo, inapaswa kulipa Sh. 5,000, kisha baba, mke na watoto wanne walio na umri chini ya miaka 18, watatibiwa kwa muda wa mwaka mmoja, bila ya kutozwa gharama zingine.
Amezitaja baadhi ya huduma zinazotolewa na mfuko huo kuwa ni pamoja na ada ya kujiandikisha na kumuona daktari, gharama ya uchunguzi wa afya, vipimo 143 na gharama za upasuaji mkubwa na mdogo.
Huduma zingine ni gharama ya dawa zote zilizoidhinishwa na wizara ya afya na ustawi wa jamii, mafao ya vifaa saidizi na huduma ya matibabu ya macho, ikiwemo pia upasuaji  husika.   

LES ENFANTS EN TANZANIE

Pour les droits des enfants en Tanzanie comme
l’education,bonne santé et bonne eleve la situation en
Tanzanie c’est contre parce que les enfants travaillent au
marche

L’enfant travailler au marche a Misungwi en Tanzanie

La photo par Eufrasia Mathias de Standard Radio FM
“La voix de sans voix”

Sunday, October 14, 2012

MBIO ZA BAISKELI SHINYANGA


Na edilitruda chami
Mkoa wa shinyanga umeendelea  kushamiri katika mashindano ya mbio za  baiskeli ambapo  chama cha wapanda biskeli katika wilaya ya shinyanga  vijijini {CHABASHI} kimeweza kuandaa mashindano ya umbali wa kilomita 35  kutoka  kijiji cha Itwangi kwenda Puni kwa kilomita 20 na kutoka itwang kwenda kituli kwa kilomita 15 ambapo washiriki  26 walijitokeza katika mbio hizo.
Juma Tagara  ndiye aliyeibuka mshindi wa kwanza, na  akazawadiwa  taslim sh. laki moja akifuatiwa na masingija ndumrli ayeliweza  kuibuka na taslim shilingi elfu sabini na mshindi wa tatu alikuwa ni Charles Clement aliejinyakulia kitita cha sh. elfu hamsini zilizotolewa na  mdhamini wa mbio hizo  Senge  Sesaguli.
Katibu wa chama cha mbio za Baiskeli wilaya ya shinyanga vijijini Shija Dalali amesema kuwa lengo la kugawa zawadi hizo kwa washindi katika mashindano hayo ni kuhamasisha vijana kushiriki katika mashindano mbalimbali  na kuhakikisha kuwa wanaibua vipaji vya wanamichezo  watakaoshiriki katika ligi mbali mbali. vijijini                                                                                                                                             
Mbali na mbio za baiskeli mkoa huo unaendesha mashindano  mbalimbali  ambapo zawadi za vitu halisi hutolewa kama vile ngombe mnyama, mbuzi mnyama, mpira wa miguu na pamoja na fedha ambazo zimekuwa zikitolewa na wadhamini mbalimbali.

MIAKA 13 YA KIFO CHA NYERERE


Ni miaka 13 sasa tangu mwalimu Julius Kambarage Nyerere aage Dunia baada ya kuugua na kulazwa katika hospitali ya St. Joseph jijini London
Katika kuadhimisha kumbukumbu ya Mwl. Nyerere mambo mengi hufanyika; miongoni mwa mambo hayo ni matembezi ya vijana, kuzima mwenge wa Uhuru pamoja na hotuba mbalimbali za viongozi wa kitaifa kuhusu Umoja na mshikamano wa watanzania
Ni dhahiri kuwa kila mtanzania analo neno la kusema kuhusu Nyerere, Wapo wanaosema kuwa Nyerere ni Baba wa Taifa, wapo wanaotamka kuwa Nyerere alikuwa mbabe na mkorofi, wapo wanaoeleza kuwa Nyerere alipenda usawa na haki kwa kila mtanzania
Standard Radio imefanya mahojiano na watu mbalimbali ili kujua nini hisia zao kuhusu mwalimu Nyerere, maoni ni mengi lakini Khadija Mahamba ambaye ni mwanachuo wa chuo cha taaluma ya Habari cha DSJ (Dar es Salaam School of Journalism) anasema kuwa Nyerere aliacha pengo kubwa nchini Tanzania
“Enzi za Mwalimu kila kitu kilikuwa kinaenda kwa usawa bila ubaguzi; lakini katika miaka 13 tangu afariki UKABILA na UDINI umeshamiri miongoni mwa watanzania

Tunapotafakari na kuadhimisha miaka hiyo ya kifo cha Nyerere ni vema basi Serikali, wanasiasa na wananchi wengine tukafikiria njia mbadala wa kutimiza malengo yetu bila kuchochea  ubaguzi, udini na kuacha ubinafsi ambao ni chanzo cha ufisadi na migogro miongoni mwa jamii yetu.” Khadija Mhamba DSJ
Standard Radio tunaunga mkono maoni haya.

Friday, October 12, 2012

UTALII NA UVIVU WA WATANZANIA


Na. Matinde  Nestory, Arusha
Leo katika safu hii tutazungumzia utalii wa ndani, ninaposema utalii wa ndani nazungumzia sisi kama watanzania tunatakiwa tujue vivutio vyetu wenyewe mfano kutembelea mbuga zetu, kupanda mlima Kilimanjaro nk.
Ukweli ni kwamba watanzania bado hawajajua umuhimu wa utalii wa ndani hii ni kutokana kwamba wageni wanakuja kutembelea vivutio vyetu lakini sisi wenye vivutio  hatuna hata hamu navyo.
Ni wazi kuwa utalii wa ndani bado haujafikia kiwango cha kueleweka,Tanzania tumebarikiwa kuwa na mbuga kama Tarangire, Serengeti, Ngorongoro, Manyara, Mikumi nk.
Katika mbuga hizo kuna wanyama ambao hawapatikani duniani kote isipokuwa Tanzania, mfano Tarangire kuna tembo wakubwa kuliko mbuga zote. Pia katika mbuga ya Tarangire kuna mibuyu mikubwa ambayo ni vivutio tosha kwa wageni ambao wanakuja na kutalii katika mbuga zetu.
Ninaweza kuthubutu kusema kuwa watanzania bado wako nyuma katika suala zima la utalii wa ndani nini tatizo linalowafanya watanzania kutokuwa na moyo wa kuvitazama vivutio vyao au kuvitembelea labda tatizo ni kiingilio cha kuingia mbugani au tatizo ni kukosa muda wa kuvitembelea, majukumu mengi au ni kuvipuuza vivutio vyao na kusubiri wageni waje na kuvitazama?
Watanzania wanatakiwa kuhamasishwa kuhusu kutembelea vivutio vyao ili waondokane na dhana ya kuwa vivutio hivyo ni vya wageni tu na kujiona wenyewe hawawezi kuvitembelea kwa kutokuelewa kwamba vivutio hivyo ni mali yao wenyewe.
Tumekuwa tukishuhudia wageni kutoka nchi mbalimbali wanakuja na kutaka kupanda mlima Kilimanjaro lakini sisi watanzania hatuna hata hamu ya kutaka  kupanda hata kidogo hata ukifika kituo cha pili katika mlima Kilimanjaro tunajua kwamba mlima Kilimanjaro upo mkoani Kilimanjaro lakini hata wazawa wa mkoa wa Kilimanjaro hawajawahi kupanda wazi ni kwamba watanzania wanatakiwa wahamasishwe kutembelea vivutio vyao.
Mwisho ninawaomba watanzania kwenda kutembelea vivutio vyao na si kusubiri wageni kutoka nje na kuja Tanzania na kujionea vivutio vyetu,pia naiomba serikali ipunguze gharama kwa wananchi wake hii itasaidia watanzania kujifunza mambo mbalimbali,na kuelewa vivutio vyao.